Adhabu ya kifo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Adhabu ya kifo duniani. Buluu: hakuna,
Kijani: Adhabu ya kifo wakati wa vita pekee; kichungwa: kuna adhabu ya kifo lakini haikutekelezwa katika miaka 10 iliyopita
Nyekundu:Adhabu ya kifo hutolewa

Adhabu ya kifo ni mauaji ya mwanadamu yanayotekelezwa na serikali baada ya mahakama imetoa hukumu ya mauti kulingana na sheria ya nchi. Kwa kawaida adhabu hii inatolewa kwa jinai nzito sana.

Sababu za kumhukumia mtu afe[hariri | hariri chanzo]

Zamani ilikuwa adhabu ya kawaida katika nchi nyingi kwa mauaji hasa, lakini pia kwa makosa kama unajisi, biashara ya madawa ya kulevya, ufisadi. Kihistoria hata aina za upinzani dhidi ya mtawala wa nchi ziliadhibiwa kwa adhabu ya mauti mara nyingi iliitwa kusaliti taifa au kuhatarisha usalama wa nchi. Kuna pia nchi ambako kuondoka katika dini rasmi iliadhibiwa hivyo.

Kwa jumla kuna hasa sababu nne zinazotajwa kwa ajili ya adhabu ya kifo:

 1. adhabu hii ni dia inayotakiwa kwa jinai nzito. Mtu aliyeua hastahili kuishi tenaa. Haki inadai ya kwamba adhabu ilingane na tendo.
 2. Adhabu ya kifo inaondoa wakosaji wenye hatari katika jamii. Hawezi kutoroka au kuachishwa jela na kuleta hatari ya kwamba atarudia matendo.
 3. Watu wengine wanaotafakari kutenda maovu yale wataogopa kufanya hivyo kwa hofu ya adhabu ya kifo hivyo hofu hii inaongeza kiwango cha usalama katika jamii.
 4. heri kumwua mkosaji aliyeua kuliko kumfunga ndani kwa maisha yake kwa sababu hii
  • inaleta gharama kubwa kwa jamii
  • ni adhabu ya kinyama zaidi kuliko kumwua mkosaji

Upinzani[hariri | hariri chanzo]

Katika karne ya 20 upinzani dhidi ya adhabu hii ilipata nguvu na nchi nyingi zimefuta adhabu ya kifo. Katika nchi nyingine adhabu iko bado kisheria lakini haikutekelezwa tena tangu miaka mingi kwa sababu katika Kenya na Tanzania.

Sababu za upinzani ni hasa kama zifuatazo:

 1. wengi hudai ya kwamba adhabu ya kifo hailingani na utu. Katika hoja hili kumwua mtu ni kinyama na hata kama mkosaji alimwua mtu mwingine na kutenda kinyama hii si sababu nzuri kwa umma au jamii kushuka chini kwenye ngazi hiyohiyo na kumtendea mksosaji jinsi alivyotenda mwenyewe.
 2. adhabu ya kifo ni adhabu ambayo haiwezi kurekebishwa. Lakini kila mahakama inaweza kukosa na kuna mifano mingi kwa kwamba mahakama ilikosa na kumhukumu mtu kuwa alihusika na jinai lakini baadaye ilionekana si yeye. Kama amefungwa jela anaweza kuachishwa na kurudishwa uhuru. Kama ameshauawa hakuna njia ya kumrudishia uhai.
 3. Hakuna uthebitisho ya kwamba adhabu ya kifo inasaidia kupunguza jinai katika jamii.

Nchi zilizotekeleza hukuma ya kifo mara nyingi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2005 watu waliuawa na serikali baada ya hukumiwa katika nchi zifuatazo:

 1. China (angalau watu 1,770)
 2. Uajemi (angalau 94)
 3. Saudi Arabia (At least 86)
 4. Marekani (60)
 5. Pakistan (31)
 6. Yemen (24)
 7. Vietnam (21)
 8. Jordan (11)
 9. Mongolia (8)
 10. Singapur (6)
 11. Uturuki (3)
 12. Ufaransa (1)

Namna za kutekeleza kifo ya mauti[hariri | hariri chanzo]

 • Kupiga risasi
 • Sindano ya sumu
 • Kunyonga
 • Kukata kichwa
 • Kiti cha umeme
 • Kurusha mawe


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Wanaopinga adhabu ya kifo[hariri | hariri chanzo]

Wanaotetea adhabu ya kifo[hariri | hariri chanzo]

MAfundisho ya kidini[hariri | hariri chanzo]