Mtaguso wa kwanza wa Vatikano
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtaguso wa kwanza wa Vatikano unatazamwa na Kanisa Katoliki kama Mtaguso Mkuu wa 20.
Uliitishwa rasmi na Papa Pius IX mnamo 29 Juni 1868 na vikao vyake viliendelea katika Basilika la Mt. Petro huko VatiKano mjini Roma kuanzia tarehe 8 Desemba 1869 hadi vilipokatika mnamo 1870. Walishiriki maaskofu na mapadri 744.
Tukio kuu la kazi hiyo ni dogma ya Papa kuwa na karama ya kutokosea katika mafundisho ya imani na maadili anayoyatoa kwa kutimiza masharti fulani (kwa kifupi: "ex cathedra", yaani "kutoka ukulu). Dogma hiyo iliimarisha mamlaka ya papa na umoja wa Kanisa dhidi ya maelekeo ya kitaifa.