Mapafu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mapafu ni sehemu ya mwili inayoingiza oksijeni mwilini na kuituma kwenda kwa seli za mwili. Ni kawaida kwa wanyama wa faila ya chordata walio na uti wa mgongo na kupumua hewa. Hutokea kwa jozi maana yake ni mapafu mawili si moja tu kama moyo.
Kuna pia samaki na konokono kadhaa wenye mapafu.
Mapafu huvuta hewa ndani ambako oksijeni ya hewa inaingizwa katika damu na kupelekwa kwenda seli za mwili. Ndani ya mapafu kuna viputo vidogo sana na hapa ni mwisho wa njia ya hewa kutoka nje. Damu inazunguka viputo hivi katika mishipa midogo inayotenganishwa na nafasi ya hewa kwa ngozi nyembamba sana. Oksijeni inaweza kupita kwenye ngozi na kuingia katika damu inapopokelewa na seli za damu nyekundu.
Chordata walio wengi huwa na mapafu mawili.
Mapafu ni sehemu ya mwili ya lazima kwa sababu seli zinakufa bila oksijeni.
[hariri] Viungo vya Nje
- A revision site directed towards IGSCE students
- A to Z list of diseases of the Lung
- List of Lung Cancer information sites
- In depth articles on the lung
- In depth article on the anatomy of a lung
| Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mapafu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
