Pomboo
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Pomboo | ||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Pomboo
|
||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Pomboo ni wanayama wa bahari wa familia mbalimbali katika oda ya Cetacea au nyangumi. Wanahesabiwa kati ya nyangumi wenye meno (Odondoceti). Spishi nyingi zinaishi baharini lakini kuna pia spishi chache wanaokaa kwenye maji matamu ya mito. Kuna pia spishi za pomboo wa mtoni ambao ni familia tofauti hata wakifanana sana na pomboo za kawaida.
Kama nyangumi wote wana maisha yanayofanana na samaki lakini si samaki bali mamalia wanaozaa watoto hai na kuwanyonyesha maziwa kwa kutumia viwele vyao. Wana damu moto na kupumua kwa mapafu maana yake hawawezi kukaa chini ya maji muda wote kama samaki wanapaswa kufika kwenye uso wa maji na kupumua kabla ya kuzama chini tena kwa muda mrefu.
Pomboo wanahesabiwa kati ya wanyama wengi akili kubwa; aina kadhaa wana ubongo mkubwa sawa na mwanadamu.
[hariri] Picha
| Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pomboo kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |