Majadiliano:Papa

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Papa - Cheo au jina?[hariri chanzo]

Papa ni cheo si jina ninavyoelewa. Majina ya mapapa ni kama vile Benedikto, Yohane Paulo na kadhalika. Kila mmoja huitwa "Papa" si kama jina lakini kama cheo. --Kipala 13:12, 2 Desemba 2007 (UTC)[jibu]


Nimerudisha mabadiliko ya mtumiaji:196.45.46.171; tumekuwa tayari na amjadiliano ya kwamba papa si jina bali cheo. Badiliko "kuchaguliwa na makardinali wa Kanisa la Roma" haieleweki; hali halisi anachaguliwa na mardinaliy a kanisa katoliki hata kama katika sheria ya kanisa katoliki makardinali hutazamiwa kama mapadre n.k. wa kanisa la mji wa Roma. Lakini hii ni jambo la ksheria ianyoweza kuelezwa katika sentensi ya pekee jinsi ilvyowekwa itachanganya wasomaji. Bdiliko kuhusu Wakopti hailingana na utaratibu wa kutosimama upande mmoja; cheo cha kiongozi huyu si "askofu" wa Aleksandria bali "papa wa Aleksandria" na hata hii si jina bali cheo. --Kipala (majadiliano) 11:37, 8 Oktoba 2008 (UTC)[jibu]

Ndugu, katika Kanisa Katoliki Papa ni jina la heshima linalotumika kwa maana ya baba. Si askofu wa Roma tu, bali hata mapadri katika baadhi ya lugha (k.mf. Kialbania cha Italia) wanaitwa hivyo. Cheo cha Benedikto XVI ni kuwa askofu (wa Roma). Hakuna daraja ya juu kuliko ile ya askofu. Benedikto ni jina lake binafsi, papa ni jina la jumla kwa yeyote anayeshika nafasi hiyo kabla au baada yake. Lakini si lazima kumuita hivyo. Wala si jina asili ya Kiitalia (baba anaitwa babbo au papa', si papa). Kuhusu makardinali, kama ulivyosema, usahihi ni kwamba ni wa Kanisa la Roma. Wanamchagua askofu wa Roma kama wawakilishi wa jimbo hilo, si wa maaskofu wa Kanisa Katoliki duniani. Kwetu ni suala la imani. Shenuda III wa Aleksandria ni askofu wa jimbo hilo, ndiyo maana anaitwa pia patriarch au papa. Naomba tena tusipotoshe habari ili kulinganisha na mitazamo ya watu wa kawaida, kama ile ya kwamba kanisa la Mt. Petro ni kanisa kuu la Roma: haijawahi kuwa hivyo, hata kama watu wanadhani hivyo. Mimi ni padri mkatoliki mzaliwa wa Roma, siwezi kushindwa kujua kanisa kuu la jimbo langu asili! Lakini usiponiamini, soma kurasa za wikipedia katika lugha nyingine kuhusu Kanisa la Laterano. Shalom! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:19, 9 Oktoba 2008 (UTC)[jibu]

Asante kwa maelezo. Kwa bahati mbaya sioni ya kwamba unajaribu kutofautisha kati ya "jina" na "cheo". Kama neno linamtaja yeyote anayeshika nafasi - je hii si cheo? Kwa Kiswahili hakuna mwingine anayeitwa "Papa" nje ya Papa wa Roma na mkuu wa kanisa la kikopti (usiponiamini- tembelea Wakopti Nairobi na kuwauliza - Tanzania wako Mara lakini sina uhakika wapi). Nakubali ya kwamba matumizi ya papa kwa askofu wa Roma ilianza kama jina la heshima kihistoria lakini tangu karne nyingi imekuwa cheo kabisa. Soma Kilatini cha "dictatus papae" - hapa neno ni cheo tayari; kwa Kilatini inaitwa "nomen" ila tu tukitofautisha jina na cheo ni cheo kamili. Si cheo chake cha pekee kuna vingine pia; kuna vitabu kadhaa juu ya vyeo vya Papa kama vile pontifex n.k. Mfano wa jina la heshima ambalo si cheo ni "baba" kama askofu, padre au mchungaji anaitwa hivyo. Papa ni tofauti.
Ombi langu ni kama jambo limenza kujadiliwa (kama hapa juu Desemba 2007) ni vema kuijadili kwanza kabla ya kubadilisha tu. Kujadili kwanza inapunguza tatizo la kutoelewana. Ningekuuliza kwanza lakini inaonekana ulibadilisha bila kujiandikisha. Mabadiliko ya jambo lililowahi kujadiliwa bila kuema kitu si njia nzuri hasa kama anayebadilisha ni mtu bila jina.
Kuhusu "Kanisa Kuu" sielewi; nilifikiri ya kwamba tulielewana. Niliomba ulete neno lingine kwa "cathedral" na kama nimeelewa vema wewe uliandika ya kwamba hakuna faida kuingiza maneno kama "katedrali" kama "kuna jina sahihi kabisa la Kiswahili: Kanisa Kuu" (ling. Talk:Kanisa Kuu la Mt. Petro. Naomba unifafanulie! --Kipala (majadiliano) 14:47, 9 Oktoba 2008 (UTC)[jibu]

Ndugu, kwanza samahani kwa kurekebisha bila kujibu maswali yako ya mwaka jana (nimeyaona baadaye tu) wala kuingia akaunti (nilisahau kama inavyokutokea wewe pia). Ni kweli kama ni vema kufuata taratibu na kudumisha uelewano katika kazi yetu hii. Kuhusu neno papa, naendelea kuliona jina la heshima sawa na baba, mhashamu, n.k. Kuhusu Wakopti, kwamba wanamuita hivyo Shenuda III ni thibitisho ya hilo, kwa sababu kwao Papa wa Aleksandria ni Patriarch wa kiti cha Mt. Marko tu, si wa Kanisa lote duniani anavyodai kuwa askofu wa Roma. Kwamba wako Nairobi na Mara labda unawachanganya na Waorthodoksi (Wamelkiti) wa Upatriarki wa Aleksandria, ambao wana ushirika na Konstantinopoli na kutenganika na Wakopti tangu mwaka 451. Hao wapo sehemu mbalimbali Tanzania na wanazidi kuenea. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 18:39, 10 Oktoba 2008 (UTC)[jibu]

Riccardo, bila samahani! Sasa sijui kama labda tatizo letu ni lugha ya Mama kichwani tukiandika Kiswahili. Nikisema Kiingereza au Kijerumani tofauti kati ya "jina" na "cheo" ni jambo lenye maana. Kiitalia sijui; Kiswahili nadhani ni tofauti pia lakini kwangu ni lugha ya pili tu. Upande wa Kanisa la Mt Petro kwangu ni tatizo hilihili; maana Kijerumani naona "Petersdom" na "Dom" ni katedrali au "kanisa Kuu". Kwa hiyo ilikuwa kosa langu. Hata kama wewe uliandika tusitumie neno "basilika" labda ionyeshwe katika makala na kuongeza makala mafupi ya "Basilika" maadamu tukieleza habari hizi neno litasaidia.
Kuhusu Wakopti sidhani ya kwamba nimewachanganya. Nairobi nimewatembelea mara kadhaa wako Ngong Road na kuhusu Mara tazama [1]. Kumbe Wamelkiti wa Antiokia wako pia TZ? Ajabu kwa sababu huko Misri ni wachache mno; nisipokosei kuna matawi kaaa ya kanisa katoliki huko yaani Kiroma (=Kilatini), Kikopti-katoliki na Melkiti (=Kigiriki-Katoliki); pia Waarmenia-Katoliki lakini wamepungua sana. Hali halisi kama makala ni kuhusu "Papa" kuna njia mbili: Ama makala za pekee kwa makanisa yanayotumia cheo hiki au makala moja itakayoeleza hasa habari muhimu za Papa wa Roma na kutaja kando cheo hiki katika kanisa la Kikopti halafu pia katika Legio Maria (Kenya hasa). Basi sitajibu kwa wiki mbili kwani nasafiri kwenda Uswahilini! --Kipala (majadiliano) 20:52, 10 Oktoba 2008 (UTC)[jibu]

Asante kwa taarifa kuhusu Wakopti wa Afrika Mashariki: kweli ni wenyewe! Nafurahi kusikia tunao jirani. Kuhusu Wamelkiti, si wale wa Antiokia, wala wale wa Yerusalemu, bali wale wa Aleksandria. Tanzania wana majimbo mawili, Dar es Salaam (wanasema Irinopoli) na lingine kwenye ziwa Viktoria. Si Wakatoliki: Wamelkiti Wakatoliki Afrika wako Misri na Sudan tu. Kuhusu ukurasa wa Papa, nitaendelea kufikiria. Kwa sasa nafurahi kwamba tumemaliza kuingiza katika wiki kurasa juu ya vitabu vyote vya Biblia. Safari njema! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 21:13, 10 Oktoba 2008 (UTC)[jibu]