Papa Yohane Paulo I
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papa Yohane Paulo I (17 Oktoba, 1912 – 28 Septemba, 1978) alikuwa papa kwa siku 33 tu kuanzia 26 Agosti, 1978 hadi kifo chake.
Mzaliwa wa Italia Kaskazini, jina lake la awali lilikuwa Albino Luciani.
Baada ya kuchaguliwa na makardinali wenzake, alijitajia jina linalounganisha yale ya mapapa wawili waliomtangulia (Papa Yohane XXIII, halafu Papa Paulo VI) ili kuonyesha nia yake ya kuendeleza kazi yao, hasa Mtaguso wa pili wa Vatikano. Ilikuwa mara ya kwanza kwa papa kuchagua jina dabo.
Ingawa muda haukumruhusu kutekeleza mipango yake, aliacha kumbukumbu nzuri ya wema wake ("papa wa tabasamu").
Aliyechaguliwa badala yake alijitajia jina hilohilo Papa Yohane Paulo II na kujiwekea lengo hilohilo.
| Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Yohane Paulo I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |