Papa Gregori VII
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papa Gregori VII (kati ya 1020 na 1025 – 25 Mei, 1085) alikuwa papa kuanzia 22 Aprili, 1073 hadi kifo chake ugenini. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Ildebrando da Soana. Alimfuata Papa Alexander II akafuatwa na Papa Victor III.
Baada ya kuwa mmonaki alichangia urekebisho wa Kanisa kama kardinali.
Kisha kuchaguliwa kuwa papa alipigania kwa nguvu zote uhuru wa Kanisa Katoliki dhidi ya mamlaka ya serikali, akifungua njia kwa mapapa waliofuata.
Alitangazwa na Papa Gregori XIII kuwa mwenye heri (1584), halafu (1728) kuwa mtakatifu na Papa Benedikto XIII.
[hariri] Maandishi yake
Barua zake nyingi kwa mtetezi wake, Matilda wa Toscana zinapatikana katika:
[hariri] Marejeo
- Cowdrey, H.E.J. (1998). Pope Gregory VII: 1073–1085. Oxford and New York: Clarendon Press.
- Emerton, Ephraim (1932). The correspondence of Pope Gregory VII: Selected letters from the Registrum. New York: Columbia University Press. OCLC 1471578.
- Robinson, Ian Stuart. (1978). Authority and Resistance in the Investiture Contest: the Polemical Literature of the Late Eleventh Century. Manchester University Press.
[hariri] Viungo vya nje
Papa Gregori VII katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki
| Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Gregori VII kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
