Mwenye heri
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwenye heri ni jina la heshima analopewa Mkristo wa Kanisa Katoliki baada ya kufa na ya kufanyiwa kesi makini kuhusu ushujaa wa maadili yake yote na juu ya muujiza mmoja uliofanywa na Mungu kwa maombezi yake baada ya kifo chake.
Kwa mfiadini inatosha kushuhudia kwa hakika kwamba aliuawa kwa ajili ya imani au adili lingine.
Asili ya hatua hiyo ni karne XIV ambapo Papa alianza kukubali marehemu aheshimiwe kwa namna ya pekee mahali fulani au katika shirika fulani kabla kesi ya kumtangaza mtakatifu haijakamilika.