Papa Benedikto IX

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Picha:B Benedikt IX.jpg
Papa Benedikto IX

Papa Benedikto IX (takriban 1012 – baada ya 1055) alikuwa papa mara tatu, kwanza kuanzia Oktoba 1032 hadi Septemba 1044, ya pili kuanzia Aprili hadi Mei 1045, na ya tatu kuanzia Novemba 1047 hadi Julai 1048. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Theophylactus. Alimfuata kwanza Papa Yohane XIX, ya pili Papa Silvester III, na ya tatu Papa Klementi II. Kila mara alifukuzwa upapani kwa ajili ya matendo yake maovu. Mwaka wake wa kufariki haujulikani kwa uhakika. Mapokeo mbalimbali yanataja mwaka wa 1055, wa 1065 au wa 1085.

Pope.svg Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Benedikto IX kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.