Askofu mkuu
Kutoka Wikipedia
Askofu mkuu ni cheo cha askofu kiongozi anayesimamia maaskofu katika jimbo la kanisa lenye dayosisi mbalimbali.
Asili ya neno lenyewe ni Kigiriki αρχή arché (mwanzo, wa kwanza). Sehemu ya pili ni neno la Kigiriki επίσκοπος episkopos (mwangalizi) lililofikia Kiswahili kupitia umbo la Kiarabu uskuf.
[hariri] Kanisa katoliki
Kama nchi ina wakatoliki wengi kuna majimbo mbalimbali na kila moja ina askofu mkuu wake. Kama idadi ya wakatoliki ni wastani huwa na jimbo moja na askofu mmoja tu mwenye cheo cha askofu mkuu.
[hariri] Waanglikana na Waluteri
Katika makanisa mengine huwa askofu mkuu ni askofu kiongozi wa nchi fulani. Lakini cheo hiki hakitumiwi vile katika kila nchi na Waluteri ni hasa Waluteri wa Uswidi, Ufini, Urusi na Estonia walio na askofu mkuu.

