Nenda kwa yaliyomo

Nchi inayoendelea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Nchi zinazostawi)

Nchi inayoendelea ni neno linalotumika kuashiria taifa lenye kiwango cha chini cha nyenzo za uendelezi. Hakuna ufafanuzi hata mmoja wa neno hilo unaokubalika kimataifa, na viwango vya maendeleo vinaweza tofautiana kati ya nchi zinazosemekana kuwa zimeendelea, huku baadhi ya nchi zinazoendelea zikiwa na viwango vya juu vya maisha.[1][2]

Baadhi ya mashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia hutumia uainishaji wa kihesabu pekee. Benki ya Dunia huchukulia nchi zote zenye mapato ya chini na ya wastani kama "zinazostawi". Katika uainishaji wake wa hivi karibuni, uchumi wa nchi uligawanywa kwa kutumia Pato la Taifa kwa kila mwananchi. Mwaka wa 2008, Pato la Taifa kwa kila mwananchi chini ya $ 11,905 zilihesabiwa kama zinazostawi[3]. Taasisi nyingine hutumia fasili zisizokuwa maalumu sana.

Nchi zenye uchumi ulioendelea zaidi kuliko nyingine zinazoendelea, lakini ambazo bado hazijaonyesha kikamilifu ishara za nchi iliyostawi huwekwa pamoja katika kundi la nchi zenye viwanda vingi. [4] [5][6] [7]

Ufafanuzi

[hariri | hariri chanzo]
2021-22 UN Human Development Report

Kofi Annan, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alifafanua nchi iliyostawi kama ifuatavyo: "Nchi iliyostawi ni nchi ambayo inaruhusu wananchi wake wote kufurahia maisha ya uhuru na afya katika mazingira salama." [8] Lakini kulingana na Divisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa,

Hakuna mfumo uliowekwa wa kutoa jina la "iliyostawi" na "inayostawi" kwa nchi au maeneo katika mfumo wa Umoja wa Mataifa. [2]

Na inabainisha kuwa

Kuweko kwa majina "iliyostawi" na "inayostawi" kuna lengo la kurahisisha shughuli za kufanya takwimu na si lazima kuhukumu hatua ilizopiga nchi au eneo fulani katika mchakato wa maendeleo[9].

Umoja wa Mataifa unabainisha pia

Katika mazoea ya kawaida, Japan katika Asia, Kanada na Marekani kaskazini mwa Amerika, Australia na New Zealand katika Oceania, na Ulaya zinachukuliwa kama kanda au maeneo "yalizostawi". Katika takwimu za biashara ya kimataifa, Shirika la Forodha la Africa Kusini pia huchukuliwa kama eneo lililostawi na Israeli kama nchi iliyostawi; nchi zinazotokana na Yugoslavia ya zamani, isipokuwa Slovenia, huchukuliwa kama nchi zinazostawi; na nchi za Ulaya mashariki na Jumuiya ya Mataifa Huru (code 172) Ulaya hazijajumuishwa aidha kama zilizostawi au zinazostawi[10].

Kulingana na uainishaji wa IMF kabla ya Aprili 2004, nchi zote za Ulaya Mashariki (pamoja na nchi za Ulaya ya Kati ambazo zimo katika "Kikundi cha Ulaya Mashariki" katika taasisi za UN) pamoja na Umoja wa Kisovyeti (USSR) nchi za Asia ya Kati (Kazakhstan, Uzbekistan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Turkmenistan) na Mongolia, hazikujumuishwa katika aidha maeneo yaliyostawi au yanayostawi, bali zilijulikana kama "nchi katika mpito"; hata hivyo kwa sasa huonekana (katika ripoti za kimataifa) kama "nchi zinazostawi".

Katika karne ya 21 kundi la awali la Four Asia Tigers [11] (Hong Kong, [11] [12] Singapore, [11] [12] Korea ya Kusini, [11] [12] [13] [14] na Taiwan [11] [12] ni kufikiriwa "yaliyoendelea" kanda au maeneo, pamoja na Kupro, [12] Israeli, [12] Malta, [12] na Slovenia, [12] ni kufikiriwa "nchi mpya zilizoendelea".

IMF hutumia mfumo wa uainishaji unaozingatia: "(1) kiwango cha mapato per capita, (2) mauzo ya mseto, na (3) shahada ya ushirikiano katika mfumo wa kifedha wa kimataifa. [15]

Benki ya Dunia huainisha nchi katika vikundi vinne vya mapato. Nchi za mapato ya chini zina Pato la Taifa kwa Kila mwananchi la US $ 975 au chini. Mapato ya chini katikati ni nchi zenye Pato la Taifa kwa Kila mwananchi la US $ 976 - $ 3,855. Nchi za Mapato ya Juu katikati ni nchi zenye Pato la Taifa kwa Kila mwananchi la US $ 3,856 - $ 11,905. Nchi za mapato ya Juu ni zile zenye pato zaidi ya $ 11,906. Benki ya Dunia huainisha nchi zote zenye mapato ya katikati na ya chini kama zinazostawi lakini inabainisha kuwa, "Matumizi wa neno hili ni kwa kurahisisha kazi tu; na hayakunuiwa kuashiria kuwa nchi zote katika kundi hilo zinapata maendeleo sawa au kwamba nchi zingine zimefikia kiwango kinachotakikana au mwisho wa hatua za maendeleo. Uainisho kwa mapato haumaanishi hicho ndicho kiwango haswa cha maendeleo kwa wakati huu[3].

Vipimo na dhana ya maendeleo

[hariri | hariri chanzo]

Maendeleo ya nchi hupimwa kwa kutumia takwimu kama vile mapato kwa Kila mwananchi (GDP), urefu unaotarajiwa wa maisha, kiwango cha kujua kusoma na kadhalika. UN imeanzisha HDI, kiashiria cha jumla cha takwimu zilizotolewa hapo juu, ili kupima kiwango cha maendeleo ya katika nchi mahali takwimu zinapatikana.

Nchi zinazostawi kwa ujumla huwa ni nchi ambazo hazijapata mafanikio muhimu katikaa sekta ya viwanda ikilinganishwa na idadi ya raia wake, na ambazo, mara nyingi huwa na hali ya wastani au chini ya kiwango cha maisha. Kuna uhusiano mkubwa kati ya mapato ya chini na kiwango cha juu cha ukuaji wa idadi ya watu.

Maneno yanayotumika kujadili nchi zinazostawi hurejelea nia na miundo ya wanayoyatumia maneno haya. Maneno mengine yanayotumiwa wakati mwingine ni nchia ambazo hazijaendelea sana (LDCs), nchi ambazo zimeendelea kidogo zaidi (LEDCs), "mataifa yasiyoendelea" au mataifa ya Dunia ya Tatu na "mataifa ambayo hayajastawi kiviwanda". Kinyume na hayo, upande ule mwingine unaitwa nchi zilizostawi, nchi zilizoendelea zaidi kiuchumi (MEDCs), mataifa ya Dunia ya Kwanza na "mataifa yaliyostawi kiviwanda".

Ili kudhibiti neno la tasfida la zinazostawi, mashirika ya kimataifa yameanza kutumia neno Nchi ambayo haijastawi kiuchumi (LEDCs) kwa mataifa maskini ambayo hayawezi kuonekana kama yanayostawi. Yaani, LEDCs ndio kundi maskini zaidi kati ya LDCs. Hii inaweza kudhibiti dhidi ya imani kuwa kiwango cha maisha katika nchi zote zinazostawi ni sawa.

Dhana ya taifa linalostawi inapatikana, chini ya neno moja au lingine, katika mifumo ya kinadharia kadhaa yenye mitazamo tofauti - kwa mfano, nadharia za ukombozi kutoka ukoloni, teolojia ya ukombozi, Umarksi, kupinga ubeberu, na uchumi wa kisiasa.

Mapungufu ya neno 'nchi inayostawi'

[hariri | hariri chanzo]

Kuna ukosoaji kwa matumizi ya neno 'nchi inayostawi'. Jina hilo linadokeza kuwa chini kwa 'nchi inayostawi' ikilinganishwa na 'nchi iliyostawi', ambalo nchi nyingi kama hizo hazipendelei. Huchukulia kuna haja ya 'kustawi' kwa mtazamo wa 'Magharibi' wa maendeleo ya kiuchumi ambayo nchi nyingi, kama vile Cuba, zimechagua kutofuata. Hivyo basi Cuba inabakia kuainishwa kama nchi 'inayoendelea' kutokana na pato lake dogo la taifa lakini ina kiwango cha chini cha vifo vya watoto wachanga na kiwango cha elimu cha juu kuliko Marekani[16].

Neno 'inayostawi' linadokeza kuwa na mwendo na haibainishi kwamba maendeleo yanaweza kuwa yanashuka au kusimama katika baadhi ya nchi, hasa zile za kusini mwa Afrika yaliyoathirika zaidi na VVU / UKIMWI.

Jina hili linadokeza usawa kati ya nchi hizo ambazo zinatofautiana sana. Pia linadokeza usawa katika nchi hizo ilhali utajiri na afya vya vikundi vilivyo tajiri na maskini vinatofautiana sana.

Hakuna kitu kama nchi zinazoendelea na zilizoendelea katika Umoja wa Mataifa, lakini kuna Faharisi ya Maendeleo ya Binadamu, ambayo imejumuishwa Katika Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, iliyoandaliwa kwa msingi wa tathmini ya Umoja wa Mataifa ya 2021 na kuchapishwa mnamo Septemba 8, 2022.[17] Ramani hii inaonyesha nchi zilizo na Faharisi ya Juu Sana ya Maendeleo ya Binadamu (nchi zilizoendelea) zilizoangaziwa kwa rangi nyeusi zaidi, na kwa Faharisi ya Maendeleo ya Binadamu ya kati na ya chini (inayoendelea) — nyepesi na ya chini kabisa (iliyoendelea kidogo) — nyepesi zaidi.

Orodha ya nchi zinazoibukia na zinazostawi (kulingana na toleo la IMF)

[hariri | hariri chanzo]
Uainishaji wa IMF na Umoja wa Mataifa; buluu: nchi zilizoendelea, chungwa: nchi zinazoendelea; nyekundu: nchi zinazobaki nyuma; kijivu: nchi zisizopangwa katika kundi lolote.

Nchi zifuatazo zinachukuliwa kama zinazoibukia na kustawi kiuchumi kulingana na ripoti ya mtazamo wa uchumi wa dunia ya Shirika la Fedha la Kimataifa ya Oktoba 2009[18].

Nchi zinazostawi ambazo hazikutajwa na IMF

[hariri | hariri chanzo]

Uainishaji na majina ya nchi

[hariri | hariri chanzo]

Nchi mara nyingi huwekwa ndani ya makundi manne hafifu ya maendeleo. Kila kikundi kinajumuisha nchi zilizotajwa katika makala yake. Neno "taifa linalostawi", sio lebo ya aina maalumu au sawa ya tatizo.

  1. Nchi zilizostawi kiviwanda hivi karibuni (NICs) ni mataifa ambayo uchumi wake una maendeleo ya juu zaidi kuliko yale yaliyo katika nchi zinazostawi, lakini bado bila ishara kamili za maendeleo ya nchi.[4][5] [6][7] NIC ni kikundi katikati ya nchi zinazostawi na zilizostawi. Kinajumuisha Brazil, Jamhuri ya Watu wa China, India, Malaysia, Mexico, Ufilipino, Afrika Kusini, Thailand na Uturuki.
  2. Masoko Makubwa yanayojitokeza (BEM), lebo yenye maana kadhaa. Jeffrey Garten alitambua, Brazili, Argentina, Mexico, Afrika Kusini, Poland, Uturuki, India, Indonesia, Jamhuri ya Watu wa China, na Korea Kusini kama mataifa ya BEM kumi bora.
  3. Nchi zenye muda mrefu wa vita vya wenyewe kwa wenyewe au kuvunjika pakubwa kwa utawala wa sheria ( "nchi zilizofeli") (km Afghanistan, Haiti, Pakistan, Somalia, Myanmar, Iraq, Zimbabwe) au zilizo na udikteta usiojali maedeleo(Korea Kaskazini) .
  4. Baadhi ya nchi zinazostawi zimeainishwa kama "nchi zilizostawi" kama vile Afrika Kusini na Uturuki na CIA; na Antigua na Barbuda, Bahamas, Bahrain, Barbados, Brunei, Estonia, Guinea ya Ikweta, Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia, na Trinidad na Tobago kuainishwa hivyo na Benki ya Dunia.
  1. Sullivan, Arthur (2003). Economics: Principles in Action. Upper Saddle River, New Jersey 07458: Prentice Hall. uk. 471. ISBN 0-13-063085-3. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-12-20. Iliwekwa mnamo 2021-02-24. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: location (link)
  2. 2.0 2.1 "Composition of macro geographical (continental) regions, geographical sub-regions, and selected economic and other groupings (footnote C)". United Nations Statistics Division. revised 17 Oktoba 2008. Iliwekwa mnamo 2008-12-30. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help)
  3. 3.0 3.1 "Country Classification". Benki ya Dunia. Iliwekwa mnamo 20 Julai 2009.
  4. 4.0 4.1 Paweł Bożyk (2006). "Newly Industrialized Countries". Globalization and the Transformation of Foreign Economic Policy. Ashgate Publishing, Ltd. ISBN 0-75-464638-6.
  5. 5.0 5.1 Mauro F. Guillén (2003). "Multinationals, Ideology, and Organized Labor". The Limits of Convergence. Princeton University Press. ISBN 0-69-111633-4.
  6. 6.0 6.1 Waugh, David (3rd edition 2000). "Manufacturing industries (chapter 19), World development (chapter 22)". Geography, An Integrated Approach. Nelson Thornes Ltd. ku. 563, 576–579, 633, and 640. ISBN 0-17-444706-X. {{cite book}}: Check date values in: |year= (help)
  7. 7.0 7.1 Mankiw, N. Gregory (4th Edition 2007). Principles of Economics. ISBN 0-32-422472-9. {{cite book}}: Check date values in: |year= (help)
  8. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-08-08. Iliwekwa mnamo 2010-01-04.
  9. http://unstats.un.org/unsd/methods/m49/m49.htm
  10. "Composition of macro geographical (continental) regions, geographical sub-regions, and selected economic and other groupings (footnote C)". United Nations Statistics Division. revised 17 Oktoba 2008. Iliwekwa mnamo 2008-12-30. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help)
  11. 11.0 11.1 11.2 11.3 11.4 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-24. Iliwekwa mnamo 2010-01-04.
  12. 12.0 12.1 12.2 12.3 12.4 12.5 12.6 12.7 [28] ^ IMF Advanced Economies List.World Economic Outlook, Database-WEO Groups and Aggregates Information, Aprili 2009.
  13. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-17. Iliwekwa mnamo 2010-01-04.
  14. http://www.ft.com/cms/s/0/98c62f1c-850f-11dd-b148-0000779fd18c.html
  15. "Q. How does the WEO categorize advanced versus emerging and developing economies?". International Monetary Fund. Iliwekwa mnamo 20 Julai 2009.
  16. "The World Factbook". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-08-12. Iliwekwa mnamo 2010-01-04.
  17. https://hdr.undp.org/content/human-development-report-2021-22
  18. IMF Emerging and Developing Economies List.World Economic Outlook Database, Oktoba 2009.
  19. 19.0 19.1 19.2 [133] ^ World Economic Outlook, International Monetary Fund, Aprili 2009, aya ya pili, Mpya 9-11.