Mataifa Yanayostawi ya G20
G20 (Kikundi cha memba 20, pia G21, G22 na G20 +) ni kambi ya mataifa yanayostawi iliyoanzishwa tarehe 20 Agosti 2003.
Kundi hili liliibuka katika mkutano wa tano wa Mawaziri wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), uliofanyika mjini Cancun, Mexico kuanzia 10 Septemba hadi 14 Septemba mwaka 2003.
G-20 ina asilimia 60 ya watu wote duniani, asilimia 70 ya wakulima na asilimia 26 ya mauzo ya kilimo duniani [1]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Chanzo chake kilikuwa mwezi Juni 2003, ambapo mawaziri wa kigeni kutoka Brazili, India na Afrika ya Kusini walitia saini tamko lijulikanalo kama Tamko la Brasilia [2] ambapo walidai kuwa
- "washirika wakuu wa biashara bado wanaadhiriwa na shaka ya kulinda kwenye sekta zenye ushindani mdogo za mataifa yao [...] na kutilia mkazo umuhimu wa matokeo ya duru ya sasa ya mazungumzo ya biashara hasa kwa kutoa sera ya kulinda na mazoea ya kuharibu biashara [...] Aidha mataifa ya Brazili, India na Afrika Kusini yaliamua kuweka pamoja mipango yao ya biashara huru."
Kwa sasa, Kikundi hiki kinajumuisha mataifa 23 : |
Hata hivyo, muonekano "rasmi" wa G-20 ulitokea kama jibu kwa nakala iliyotolewa tarehe 13 Agosti 2003 na Jumuiya ya Ulaya (EC) na Marekani iliyokuwa na pendekezo sawa la kilimo kwa mkutano wa mawaziri mjini Cancun.
Mnamo tarehe 20 Agosti 2003, hati iliyotiwa saini na nchi ishirini na kutolewa tena kama hati ya mkutano wa mawaziri wa Cancun mnamo tarehe 4 Septemba ilipendekeza mbadala kiunzi kwa ule wa EC na Marekani kuhusu kilimo kwa mkutano wa Cancun.
Hati hii iliashiria mwanzo wa G-20. Wasajiliwa wa awali wa kundi, kwenye hati ya 20 Agosti 2003, walipitia mabadiliko mengi, huku wakijulikana kwa majina tofauti kama vile G-21 au G-22. Jina G-20 mwishowe lilichaguliwa, kwa heshima ya tarehe kikundi kilipoanzishwa.
Tangu lianzishwe, kundi hili limekuwa na uanachama usio thabiti. Wanachama wa awali walikuwa ni pamoja na: Colombia, Costa Rica, Ecuador, El Salvador, Peru, na Uturuki.
Kufikia Oktoba 2008, kundi hili lilikuwa na wanachama 23.
Msingi wa uongozi wa G-20, unaojulikana kama kambi ya G4, unajumuisha Brazili, China, India na Afrika ya Kusini.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-08-25. Iliwekwa mnamo 2010-01-19.
- ↑ IBSA - utatu, mpango wa maendeleo kati ya India, Brazil na Afrika ya Kusini
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ukurasa mwanzo wa tovuti ya G20 Archived 1 Septemba 2009 at the Wayback Machine.
- G20 tarehe 19 Machi 2005 Archived 1 Desemba 2005 at the Wayback Machine. - ujumuisha alama ya kundi
- G20, muungano wa nchi zinazoendelea Archived 15 Machi 2022 at the Wayback Machine. katika mkazo juu ya Biashara 98, Aprili 2004
- Wa G - 20: Malengo na mitazamo ya Muungano Mpya wa Biashara Archived 13 Machi 2006 at the Wayback Machine.