Tasifida

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tasfida)

Tasifida (au tasfida, kutoka neno la Kiajemi; kwa Kiingereza "euphemism") ni usemi ambao unatunza adabu kwa kutumia maneno ya staha au ya kificho badala ya kutaja wazi matusi au maneno yanayoweza kukera yakitamkwa hadharani

Mbinu hiyo hupunguza makali ya lugha kwa kuepuka maneno ya kuvunja heshima na kutumia maneno yasiyoudhi wasikilizaji.

Kwa ufupi tasifida ni matumizi ya lugha yenye heshima na adabu.

Mifano[hariri | hariri chanzo]

  1. Jamiiana - kitendo cha ngono
  2. Kwenda pembeni - kwenda haja ndogo
  3. Kwenda msalani - kwenda haja kubwa
  4. Aga dunia - kufa
  5. Mjamzito - mwanamke aliye na mimba. Mfano: Mama yake ni mjamzito.
  6. Ugua mdudu - ugua ugonjwa wa UKIMWI
  7. Kujifungua - tendo la kuzaa mwana. Mfano: Mke wangu amejifungua kimwana.
  8. Siti: Jina la heshima la mwanamke. Hutumika kabla ya jina lake. Mfano: Siti Salome ametuwekea mfano mzuri wa kuiga.
  9. Bwana: Jina la heshima kwa mwanamume. Mfano: Bwana Yesu Kristo.
  10. Hayati: Jina la heshima la kumtajia mtu mashuhuri aliyeaga dunia. Mfano: Hayati Mzee Jomo Kapingaalitawala
  11. Marehemu: Jina la heshima la kumtajia mtu aliyeaga dunia. Mfano: Mwili wa marehemu Juma umesafirishwa nyumbani.
  12. Kibibi: Tamko la kumwita mtoto mwanamke.
  13. Nana: Jina la heshima ambalo hutumiwa kumwitia mwanamke.
  14. Mwinyi: Jina la heshima ambalo hutumiwa kumwitia mwanamume.