Kisii
Jiji la Kisii | |
Mahali pa mji wa Kisii katika Kenya |
|
Majiranukta: 0°41′0″S 34°46′0″E / 0.68333°S 34.76667°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Kisii |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 83,460 |
Tovuti: www.kisii.com |
Kisii ni mji upatikanao Kusini Magharibi mwa Kenya. Huu ndio mji mkubwa wa biashara katika miinuko ya Gusii. Mji huu pia huitwa Bosongo au Getembe
Kisii ndio makao makuu ya Kaunti ya Kisii. Awali ulikuwa makao makuu ya Wilaya ya Kisii kwa ujumla kabla ya wilaya hiyo kugawanywa na kuzaa Wilaya ya Nyamira na Wilaya ya Gucha. Hata hivyo bado mji huo uliendelea kuzifaidi wilaya hizi na Nyanza kusini kwa ujumla, hasa kibiashara.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Kuna shughuli za viwanda katika mji huu na vingi vya viwanda hivi vinahusiana na kilimo kwa kuwa Kisii uko katika eneo lililotawaliwa na ukulima.
Pia kuna uchongaji wa madini katika eneo hili, hasa madini ya soapstone katika eneo la Tabaka[1].
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Kutokana na idadi kubwa ya watu (83,460 kadiri ya sensa ya mwaka 2009[2]) na ongezeko la mahitaji ya elimu, vyuo vingi vimeanzisha matawi Kisii. Miongoni mwa vyuo vilivyoanzisha matawi mjini ni:
Licha ya hivyo kuna shule nyingi za sekondari humo mjini, kama vile Shule ya Upili ya Kisii.
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Mji huu una wakazi wa matabaka mbalimbali, miongoni mwao wakiwemo Wahindi na Wakikuyu wanaojihusisha na biashara, huku idadi kubwa ikiwa Wakisii.
Hata hivyo, Wahindi wamenunua mali nyingi kutoka kwa Wakisii, ambayo wamekuza kuwa maduka makuu na jambo hili limeukuza mji huu kiajabu hivi karibuni. Leo hii mji huu unajivunia maduka makuu kama Tuskys na Nakumatt, benki kama vile Benki ya Equity, Benki ya Family, K-Rep, Benki ya Cooperative na Benki ya Barclays ambayo yote yameanzisha matawi mjini Kisii.
Hali ya usafi na nyumba
[hariri | hariri chanzo]Mji wa Kisii una kiwango cha chini cha usafirishaji wa takataka na maji machafu. Kituo pekee cha kusafisha maji machafu kilikuwa Daraja Mbili lakini kimehamishwa nje ya mji.
Mji huu pia unakumbwa na uhaba wa ardhi huku mitaa mingi mjini ikianzishwa bila mpango maalumu.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Tabaka la Kisii (Kisii Tribe)-Carvers of Soapstone in Kisii: kenya-information-guide.com Ilihifadhiwa 18 Machi 2010 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Sensa ya Kenya 2009 Ilihifadhiwa 9 Januari 2019 kwenye Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Kuhusu Gusii
- Tovuti Rasmi ya Kisii
- Lugha ya Ekegusii Ilihifadhiwa 10 Mei 2007 kwenye Wayback Machine.