Wanyakyusa
Wanyakyusa (pia huitwa Wangonde au Wasochile) ni kabila la watu wanaoishi kwenye wilaya ya Rungwe katika sehemu za kusini za Mkoa wa Mbeya (Tanzania), kaskazini kwa Ziwa Nyasa.
Lugha yao, inayoendelea kutumika sana, ni Kinyakyusa.
Mara nyingi Wagonde upande wa kusini wa mto Songwe nchini Malawi huhesabiwa pamoja nao katika kundi lilelile.
Mwaka 1993 watu zaidi ya milioni walikuwa wanajumlishwa kwa jina hili, takriban 750,000 upande wa Tanzania na 300,000 upande wa Malawi.
Historia
Kihistoria watu wanaoitwa leo Wanyakyusa waliitwa Wakonde, ambao kati yao Wanyakyusa walikuwa ndio kabila kubwa. Wakati wa karne ya 20 "Wanyakyusa" limekuwa jina la kundi kwa jumla.
Hadi leo kanisa la Kilutheri la KKKT linatumia jina "dayosisi ya Konde" kwa eneo lake katika mkoa wa Mbeya.
Wakati Wajerumani walipofika sehemu za kaskazini kwa Ziwa Nyasa mwisho wa karne ya 19 hawakuona tofauti ya msingi kati ya watu wa Malawi kaskazini na wale wa sehemu za Rungwe wakawaita wote "Wakonde" kutokana na jina lililokuwa kawaida ziwani.
Mgawanyiko wa Wanyakyusa
Wanyakyusa toka zamani walijulikana kama watu wa Konde. Wengi walikuwa kaskazini kwa ziwa Nyasa, lakini katika harakati za maisha na mabadiliko ya mazingira wengi wao wakakimbilia Mbeya mjini na sehemu nyingine.
Pamoja na hayo, hasa Wanyakyusa wapo wa aina mbili nao ni: Wanyakyusa wa Tukuyu na Wanyakyusa wa Kyela.
Sifa za Wanyakyusa wa Kyela
1. Wengi si wapole mtu afanyapo kosa
2. Wanamcha Mungu
3. Wanajua kupenda
4. Hawapendi dharau
5. Wanapenda kujulikana (hasa kama wamesoma hadi kupata digrii n.k.)
6. Ni wapiganaji sana kimaisha
7. Wana wivu katika masuala ya mapenzi
8. Wanapenda haki itendeke, hawapendi ubabaishaji
9. Ni watu shupavu sana kwenye kazi za kujitolea, hasa za kijamii
Sifa za Wanyakyusa wa Tukuyu
1. Ni wapole
2. Wanamcha Mungu
3. Wanajua kupenda
4. Hawapendi dharau kabisa
5. Wanajituma kwenye kazi, hasa kilimo
6. Wana wivu sana
7. Wanapenda haki itendeke na hawapendi ubabaishaji
8. Ni watu jasiri na wasioogopa vitisho
9. Ni welevu
Marejeo
- Arnold, Bernd. (Steuer und Lohnarbeit im Südwesten von Deutsch- Ostafrika,1891 bis 1916)
- Bauer, Andreus. (Raising the Flag of War)
- Charsley, S.R. (The Princes of Nyakyusa)
- Ileffe, John. (A Modern History of Tanganyika)
- Merensky, A. (Deutsche Arbeit am Nyaßa)
- Oliver, Roland. (Sir Harry Johnston & the Scramble for Africa)
- Tew, Mary. (Peoples of the Lake Nyasa Region)
- Wilson, Monica. (Good Company)
Viungo vya nje
- Ethnologue report: Nyakyusa
- The Nyakyusa Homepage
- "Wakonde" katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani (1920)
- Marcia Right, Nyakyusa Cults and Politics in the later Nineteenth Century; in: Ranger - Kimambo, The Historical Study of African Religion, Berkeley & Los Angeles 1972 (google book review) Archived 5 Julai 2007 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wanyakyusa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |