Wazaramo
Wazaramo ni kabila la watu kutoka eneo la Dar es Salaam, baina ya Rufiji na Bagamoyo, nchini Tanzania. Mwaka 2000 idadi ya Wazaramo ilikadiriwa kuwa 656,730 [1]. Lugha yao ni Kizaramo. Katika eneo la Rufiji wanajulikana pia kwa jina la Wamyagatwa.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Wazaramo ni sehemu ya Wabantu. Mababu wanaaminika waliingia katika eneo la Tanzania katika milenia ya kwanza BK. Historia yao ya kimdomo inasema ya kwamba walihamia pwani katika mazingira ya Dar es Salaam kutoka Uluguru (Morogoro) katika karne ya 18.
Walipokaa kwenye pwani walikuwa karibu na makazi ya Waswahili wakaanza kufahamiana na Waislamu. Taarifa za wakoloni Wajerumani mwanzoni mwa karne ya 20 zinaonyesha ya kwamba wakati ule Uislamu ulikuwa umeenea kati ya Wazaramo na waliendelea kujiunga nayo haraka. Siku hizi idadi kubwa wa Wazaramo ni Waislamu.
Jiji la Dar es Salaam lilikua haraka na kumeza vijiji vingi vya Wazaramo na wengine walihamia jijini wakitafuta kazi.
Mila na desturi
[hariri | hariri chanzo]Taarifa za mwanzo wa karne ya 20 zasema ya kuwa Wazaramo walikuwa na desturi za pekee tofauti na wakazi wengine ya pwani:
- nyumba zao zilikuwa kubwa na za umbo la mraba.
- Mazishi yalikuwa ya kulaza maiti kaburini kichwa kuelekea magharibi, mwanamume akilazwa upande wa kulia na mwanamke akilazwa upande wa kushoto.
- Kaburi lilipambwa kwa kusimamisha ubao mguuni na sanamu ya ubao yenye kofia upande wa kichwa; kaburi lote lilifunikwa kwa paa la manyasi
- Mabinti walipewa "mwanang`iti" (mwanasesere wa kike wa ubao) waliotumia kuanzia kubalehe hadi kumzaa mtoto wa kwanza.
Jambo muhimu ni kwamba, kama Waluguru, Wakaguru, Wakutu na Wakwere, kabila hilo linafuata mfumojike, yaani ukoo wa mama ndio unaoongoza familia na watoto wote wanahesabiwa kuwa wa ukoo huo.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- en: Makala ya Wazaramo katika "ethnologue.com".
- en: Zaramo Information Archived 7 Novemba 2005 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wazaramo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |