Watongwe
Watongwe ni kabila la watu kutoka eneo la Ziwa Tanganyika, Wilaya ya Kigoma Vijijini, sehemu ya magharibi ya nchi ya Tanzania. Lugha yao ni Kitongwe.
Mwaka 2000 idadi ya Watongwe ilikadiriwa kuwa 31,551 [1]. Inawezekana kwamba idadi yao ni kubwa zaidi, ila hujitokeza kama Wamanyema, wengine wanapokuwa Tabora hujiita Wanyamwezi, wakiwa Lyambalya Mfipa Wafipa, na wakiwa Uvinza Watongwe.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Watongwe baada ya kuongezeka walisogea pande za Fipa na kundi jingine lilielekea Uvinza. Walioelekea pande za Fipa waliongozwa na chifu Lulengelule ambaye alikuja kutawala eneo hilo hadi aliposogea Uvinza na makazi yake yalikuwa juu ya mlima Kasozinyanza ambapo hasa ndio panaitwa Uvinza, tofauti na Uvinza inayotambulika sasa au iliyokuja kutambulika baadae, yaani ilipo sasa katikati ya mito ya Malagarasi na Luchugi.
Uvinza ya Watongwe waliotoka Fipa iko juu ya mlima Kasozinyanza nyuma ya kiwanda cha chumvi ya kupika kwa magogo ilipo barabara ya Mpanda.
Watongwe waliopitia Tongwe ya Ilagala walifikia eneo la Nkwaza chini ya uongozi wa mwami Lubambo. Wao walikaa eneo la Nkwaza panapotoka chumvi ya kuanika juani siku hizi.
Watani wakubwa wa Watongwe ni Waha na Wagoma na kwa sehemu ndogo ni Wafipa kwani hao ni sehemu ya Watongwe baada ya kuwa chini ya utawala wa Lulengelule, hivyo wakawa ndugu. Pia wanashabihiana na Wanyamwezi kwa mambo mengi ya kimila kama ngoma za maswezi, chakula cha uyoga na nyama za pori na asali. Hivyo Mtongwe, Mnyamwezi na Mfipa huwa kama watu binamu.
Mfano wa majina ya Kitongwe, ni kama Masato, Mlela, Waleri n.k.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Watongwe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |