Nenda kwa yaliyomo

Wambugu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wambugu ni kabila linalopatikana katika wilaya ya Lushoto ambako wanaishi katika makundi katikati ya jamii ya Wasambaa. Maeneo wanakopatikana kwa wingi ni Kwemakame, Mazumbai, Kinko, Rangwi, Msare, Mavumo, Kitanga na Magamba na sehemu nyingine,

Asili ya kabila hilo ni wafugaji wa Manyara au Magugu ambao wametawanyika maeneo mengi ndani na nje ya wilaya ya Lushoto, Korogwe, Same na Bumbuli.

Idadi ya Wambugu ni asilimia ndogo tu kulingana na Wasambaa wa Lushoto. Kutokana na uchache wao lugha yao imekuwa inaingiliana sana na Kipare, hivyo lugha yao hasa wanaiita Kimbugu cha ndani. Inaonekana ngumu sana, na wenyeji wa Lushoto wanashindwa kuijua haraka.

Asili ya mbali ni Wakushi kutoka Mashariki ya Kati. Waliingia Afrika miaka kadhaa Kabla ya Kristo. Hao Wakushi ni pamoja na Wasomalia na baadhi ya Waethiopia na Waeritrea; walioko Tanzania ni hasa Wairaqw: hiyo ni jamii moja ambayo asili yake ni moja.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wambugu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.