Washambaa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wasambaa)
Jump to navigation Jump to search

Washambaa (au Wasambaa, kama wanavyojulikana sana) ni watu wa kabila kutoka eneo la Milima ya Usambara, kaskazini-mashariki mwa nchi ya Tanzania.

Mwaka 2001 idadi ya Washambaa ilikadiriwa kuwa 664,000.[1].

Washambaa wanaishi kwenye milima ya Usambara na lugha yao kubwa ni Kisambaa.

Wasambaa wamegawanyika katika koo mbalimbali ndani ya jamii zao ambazo ndizo utambulisho wao. Ukoo ni jambo muhimu sana katika maeneo ya Usambaa kwani wanajamii wa Kisambaa wanatambuana kwa majina ya ukoo.

Alama maarufu ya koo za Kisambaa ni majina yanayoanza na "She" kama Shemhina, Shekusa, Shekiango, Shekimwei, Sheiza, Shembilu, Shekinyashi, Sheshe n.k. Koo nyingi za Kisambaa zinajulikana kwa majina yao kuanza hivyo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Washambaa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.