Umoja wa Afrika : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Tags: Mobile edit Mobile web edit
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
[[Picha:Flag African Union 02.svg|thumb|200px|Bendera ya Umoja wa Afrika]]
[[Picha:Flag African Union 02.svg|thumb|200px|Bendera ya Umoja wa Afrika]]
[[Picha:Map of the African Union.svg|200px|thumbnail|right|Ramani ya Umoja wa Afrika. Nchi zote za Afrika ni wanachama (baada ya [[Moroko]] kujiunga upya tarehe [[30 Januari]] [[2017]]).]]
[[Picha:Map of the African Union.svg|400px|thumbnail|right|Ramani ya Umoja wa Afrika. Nchi zote za Afrika ni wanachama (baada ya [[Moroko]] kujiunga upya tarehe [[30 Januari]] [[2017]]).]]
'''Umoja wa Afrika (UA)''' (kwa [[Kiingereza]]: '''African Union (AU)'''; [[Kifaransa]]: '''Union Africaine (UA)'''; [[Kihispania]]: '''Unión Africana (UA) '''; [[Kireno]]: '''União Africana (UA) ''') <ref> [http://au.int/en/sites/default/files/PROTOCOL_AMENDMENTS_CONSTITUTIVE_ACT_OF_THE_AFRICAN_UNION.pdf Official Languages AU "Art. 11 AU" Protocol on amendments to the constitutive act of the African Union] </ref> ni muungano wa nchi 55 za [[Afrika]] ulioanzishwa mnamo Julai [[2002]].

Pitio la 09:20, 20 Machi 2019

Bendera ya Umoja wa Afrika
Ramani ya Umoja wa Afrika. Nchi zote za Afrika ni wanachama (baada ya Moroko kujiunga upya tarehe 30 Januari 2017).

Umoja wa Afrika (UA) (kwa Kiingereza: African Union (AU); Kifaransa: Union Africaine (UA); Kihispania: Unión Africana (UA) ; Kireno: União Africana (UA) ) [1] ni muungano wa nchi 55 za Afrika ulioanzishwa mnamo Julai 2002.

Umoja huu unaendeleza kazi za Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa Kiingereza: Organisation of African Union - OAU) uliokuwepo 1963 hadi 2002.

Nia ya umoja huu ni kujenga muundo na mfumo wa kisiasa, wa kiuchumi, na wa kijamii ili kufikia wakati ambapo bara la Afrika litakuwa na bunge moja, benki moja, jeshi moja, rais mmoja, sarafu moja, n.k.

Dhumuni kubwa la umoja huu ni kuunganisha nguvu za mataifa ya Afrika ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili bara hili kama vile vita, njaa, Ukimwi, n.k.

Nchi wanachama

Umoja wa Afrika ina nchi wanachama 55, yaani nchi zote za bara la Afrika (baada ya kurudi kwa Moroko, iliyokuwa imejiondoa mwaka 1985 kwa sababu UA ilitambua Sahara ya Magharibi kuwa nchi ya kujitegemea wakati Moroko inadai ya kwamba ni eneo la majimbo yake ya kusini). [2]Hata hivyo mwaka 2016 Moroko ilionyesha nia ya kujiunga tena na UA.[3]

Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika ulifanyika mwaka 2004 huko Afrika Kusini.

Mikutano mikuu ya UA

  1. Durban (Afrika Kusini): 9-11 Jul. 2002.
  2. Maputo (Msumbiji): 10-11 Jul. 2003.
  3. Sirte (Libya), mkutano wa dharura: Feb. 2004.
  4. Addis Ababa (Ethiopia): 6-8 Jul. 2004.
  5. Abuja (Nigeria): 24-31 Jan. 2005.
  6. Sirte (Libya): 28 Jun. - 5 Jul. 2005.
  7. Khartoum (Sudan): 16-24 Jan. 2006.

Viongozi

Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya UA ni N. Dlamini-Zuma.

Spika wa Bunge la Umoja wa Afrika ni Roger Nkodo Dang.

Tanbihi

  1. Official Languages AU "Art. 11 AU" Protocol on amendments to the constitutive act of the African Union
  2. [1]
  3. "Morocco seeks to rejoin African Union after 32 years". BBC News. 18 July 2016. Retrieved 18 July 2016.

Viungo vya nje