Benin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Benini)
Rukia: urambazaji, tafuta
République du Bénin
Jamhuri ya Benin
Bendera ya Benin Nembo ya Benin
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Fraternité, Justice, Travail
(Kifaransa: Ushirikiano, Haki, Kazi)
Wimbo wa taifa: L'Aube Nouvelle
Lokeshen ya Benin
Mji mkuu Porto Novo, Cotonou1
6°28′ N 2°36′ E
Mji mkubwa nchini Cotonou
Lugha rasmi Kifaransa
Serikali Jamhuri ya kidemokrasia
yenye vyama vingi

Yayi Boni
Uhuru
kutoka Ufaransa
1 Agosti 1960
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
114,763 km² (101st)
0.02
Idadi ya watu
 - Julai 2013 kadirio
 - 2013 sensa
 - Msongamano wa watu
 
10,323,000 2 (85th)
9,983,884
78.1/km² (120th 3)
Fedha CFA franc (XOF)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+ 1)
(UTC)
Intaneti TLD .bj
Kodi ya simu +229

-

1.) Mji wa Cotonou ni makao makuu ya serikali.
2.) Mwaka wa makadirio ni 2005.Jamhuri ya Benin ni nchi huru katika Afrika ya Magharibi. Zamani iliitwa Dahomey. Inapakana na Bahari ya Atlantiki upande wa Kusini, nchi ya Togo upande wa Magharibi, nchi ya Nigeria upande wa Mashariki na nchi za Burkina Faso na Niger upande wa Kaskazini.

Haihusiani na Mji wa Benin (Benin City) wala na Ufalme wa Benin wa karne ya 19.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Sherehe na ngoma kule Abomey, 1908.

Ufalme wa Dahomey ulianzishwa katika nchi ya kisasa ya Benin.

Katika karne ya 17, ufalme huo uliotawaliwa na oba (ni cheo cha mfalme wake) ulienea sehemu kubwa ya Afrika ya Magharibi.

Kulikuwa na utajiri mkubwa kwa sababu ya kufanya biashara na Wazungu, hasa Wareno na Waholanzi waliofika kuanzia mwisho wa karne ya 15. Pwani ya Benin ya leo ilijulikana kama Pwani ya Watumwa. Biashara ya watumwa iliendelea kwa karne tatu mpaka mwaka wa 1885.

Kuanzia karne ya 18, ufalme wa Dahomey ulidhoofika mpaka Ufaransa uliweza kuuvamia mwaka wa 1892. Dahomey ikawa chini ya ukoloni wa Ufaransa kuanzia mwaka wa 1899 hadi ilipopata tena uhuru tarehe 1 Agosti 1960.

Mpaka mwaka wa 1972 makundi mbalimbali walipigana vita, hatimaye Wakomunisti walianza kutawala chini ya kiongozi wao Mathieu Kérékou.

Hapo nchi ilipewa jina jipya, yaani Jamhuri ya Watu wa Benin, mwaka wa 1975 hadi 1991.

Tangu miaka ya 1980 nchi ilifuata mfumo wa soko huria. Kérékou alikuwa Rais hadi 1991, halafu tena miaka 1996-2006.

Katika uchaguzi wa Machi 2006, Yayi Boni alipata urais aliouanza tarehe 6 Aprili 2006.

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Siasa ya Benin

Bunge la Benin lina viti 83. Huchaguliwa kila mwaka wa nne. Rais ni mkuu wa serikali na wa nchi, naye huchaguAngalizo: Makadirio kwa nchi hiyo yamehesabu pia maafa ya ziada yaliyosababishwa na UKIMWI. Hii ingeweza kusababisha takwimu tofauti na itarajiwayo
3.)liwa kila mwaka wa tano. Mgombea urais anatakiwa asiwe na umri wa miaka zaidi ya sabini.

Majimbo[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Majimbo ya Benin

Kuna majimbo 12, nayo ni:

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Benin map.png

Nchi ya Benin iko kati ya Mto wa Niger upande wa Kaskazini na Bahari ya Atlantiki upande wa Kusini. Haina milima mirefu.

Idadi kubwa ya watu wanaishi katika tambarare za Kusini ambapo miji mikubwa ya Benin iko, ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Porto Novo, na mji mkubwa zaidi, Cotonou. Sehemu za Kaskazini ni kavu hasa.

Nchi ya Benin inapata majira mawili ya mvua, Aprili-Julai na Septemba-Novemba. Pia kuanzia mwezi Desemba, kuna upepo ulioitwa harmattan, nao huleta vumbi na baridi wakati wa usiku.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Uchumi wa Benin hauna nguvu sana, na hutegemea hasa kilimo, mazao ya pamba na biashara ndogondogo.

Demografia[hariri | hariri chanzo]

Picha kutoka kijiji cha Benin

Kuna makabila mbalimbali ambayo watu wake wanaongea lugha tofauti sana, k.m. Kihausa, lugha za Kisonghai, lugha za Kimande na lugha za Kifula.

Kabila kubwa kabisa ni lile la Wafon (39.2%).

Lugha rasmi ni Kifaransa.

Upande wa dini, Wakristo ni 42.8% (Wakatoliki 27.1%, halafu madhehebu mengi ya Uprotestanti). Waislamu ni 24.4%. Wafuasi wa dini asilia za Kiafrika 23.3% (hasa Vodun 17.3%). Asilimia 6.5 hawana dini yoyote.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Adam, Kolawolé Sikirou and Michel Boko (1983), Le Bénin. SODIMAS, Cotonou and EDICEF, Paris.

Viungo ya nje[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Benin kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.