Nenda kwa yaliyomo

Lugha za Kisonghai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lugha za Kisonghai ni kundi la lugha zenye uhusiano wa karibu sana zinazotumiwa na wasemaji takriban milioni 3 katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi.

Uenezi wa kijiografia

[hariri | hariri chanzo]

Lugha za Kisonghai zinasemwa upande wa Mto wa Niger nchini Mali, Niger, Benin, Burkina Faso, na Nijeria.

Awali, eneo hilo lilipokuwa chini ya utawala wa Dola la Songhai, lugha hizo zilikuwa zikitumiwa kama lugha ya mawasiliano katika sehemu kubwa sana.

Uhusiano wa kinasaba

[hariri | hariri chanzo]

Uhusiano wa Kisonghai na lugha nyingine ni ngumu sana kuthibitishwa kwa kuwa kina maneno mengi yenye asili nyingi mbalimbali.

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha za Kisonghai kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.