Wilaya ya Laikipia
Wilaya ya Laikipia | |
Mahali pa Wilaya ya Laikipia katika Kenya | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Mji mkuu | Nanyuki |
Eneo | |
- Jumla | 8,696.1 km² |
Idadi ya wakazi (2009 Sensa[1]) | |
- Wakazi kwa ujumla | 399,227 |
Wilaya ya Laikipia ilikuwa moja kati ya wilaya sabini na moja za Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).
Ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Bonde la Ufa iliyoko kwenye Ikweta.
Makao makuu yalikuwa mjini Nanyuki.
Kwa sasa imekuwa kaunti ya Laikipia.
Wilaya hii ilikuwa na vituo viwili vikuu vya soko: Nanyuki kwenye upande wa kusini mashariki, na Nyahururu kwenye upande wa kusini magharibi.
Wakikuyu walikuwa takribani 60% ya idadi ya watu wote kwenye wilaya hii, huku idadi iliyosalia ikijumuisha watu wa makabila mengine, ni pamoja na Mukogodo Masai, Wasamburu, Wameru, Waborana, Wakalenjin, Wasomali, Wazungu, Watu wa asili ya Asia, na Waturkana, wakiipa wilaya hii idadi ya watu tofauti tofauti. Mashamba mengi yanamilikiwa na idadi ndogo ya masetla wa ukoloni.
Shughuli kuu za kiuchumi katika wilaya hii ni utalii na kilimo, haswa mimea za mbegu, ufugaji na kilimo cha maua,matunda na mboga.
Hali ya hewa ya wilaya hii ni ya baridi kiasi, ikiwa na msimu wa mvua na kiangazi.
Serikali za Mtaa (Mabaraza) | |||
Baraza | Aina | Idadi ya Watu* | Wakaazi wa mjini* |
---|---|---|---|
Nanyuki | Manispaa | 39,838 | 31,577 |
Nyahururu | Manispaa | 32,120 | 24,751 |
Rumuruti | Mji | 31,649 | 4,249 |
Laikipia | Kaunti | 218,580 | 3,610 |
Jumla | - | 322,187 | 64,187 |
* 1999 census. Source: [1] |
Maeneo ya utawala | |||
Tarafa | Idadi ya Watu* | Wakaazi wa mjini* | Makao makuu |
---|---|---|---|
Mkoa wa Kati | 77,478 | 28,489 | Nanyuki |
Lamuria | 38,517 | 0 | Lamuria |
Mukogondo | 13,176 | 624 | |
Ngarua | 65,545 | 2,813 | Kinamba |
Nyahururu | 37,412 | 22,459 | Nyahururu |
Olmoran | 11,069 | 0 | |
Rumuruti | 78,894 | 4,061 | Rumuruti |
Jumla | 322,187 | 58,466 | - |
* 1999 census. Sources: [2], [3], |
Wilaya hii ina Majimbo ya Uchaguzi mawili: