Chad

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tchad)
Jamhuri ya Chad (Kiswahili)
Jumhuriyyat Tshad
Bendera ya Chad Nembo ya Chad
(Bendera ya Chad) (Nembo ya Chad)
Lugha rasmi Kiarabu, Kifaransa
Mji Mkuu N'Djamena
Mji Mkubwa N'Djamena
Serikali Jamhuri
Rais Vacant
Eneo km² 1,284,000
Idadi ya wakazi 13,670,084 (2015)
Wakazi kwa km² 11
Uchumi nominal Bilioni $11
Uchumi kwa kipimo cha umma $890
Pesa CFA frank (XFA) (Frank ya Afrika ya Kati)
Kaulimbiu "Umoja, Kazi, Maendeleo"
Wimbo wa Taifa Nyimbo ya Chad
Chad katika Afrika
Saa za Eneo UTC +1
Mtandao .td
Kodi ya Simu +235

Chad (pia: Chadi) ni nchi huru iliyoko Afrika ya Kati. Imepakana na Libya, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kamerun, Nigeria na Niger.

Mji mkuu ni Ndjamena.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya nchi.

Sehemu kubwa ya eneo lake ni jangwa na nchi yabisi. Kusini kuna kanda lenye hali ya hewa ya kitropiki, lakini ardhi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo ni asilimia 3 tu za eneo lake lote .

Kaskazini kuna milima ya Tibesti.

Katikati liko beseni la ziwa Chad lililokuwa kati ya maziwa makubwa kabisa duniani lakini limepungua sana, hasa mwishoni mwa karne ya 20.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Historia ya Chad

Katika milenia ya 7 KK kulikuwa na watu wengi sana katika beseni hiyo.

Katika historia kabla ya ukoloni watu wa kaskazini waliwafanyia vita watu wa kusini na kuteka wafungwa kama watumwa. Hivyo hadi leo uhusiano kati ya kusini na kaskazini ya nchi ni mgumu.

Tangu mwaka 2003 petroli imekuwa inaongoza kati ya bidhaa zinazopelekwa nje ya nchi badala ya pamba.

Tangu mwaka huo Mgogoro wa Darfur nchini Sudan umevuka mpaka na kuvuruga Chad pia. Ikiwa kati ya nchi zinazoongoza duniani kwa ufukara na ufisadi, ilipata shida kupokea wakimbizi kwa mamia elfu.

Ingawa kulikuwa na vyama vingi vya siasa na mapigano ya kisiasa pamoja na majaribio ya mapinduzi, mamlaka ilibaki imara mikononi mwa Rais Déby na chama chake, Patriotic Salvation Movement, hadi alipouawa mwaka 2021.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Msichana wa mkoa wa Ouaddaï.

Wakazi walikuwa 15,500,000 mwaka 2018.

Jinsi ilivyo katika nchi mbalimbali za kanda la Sahel kuna aina mbili za wakazi ndani yake:

Kwa jumla leo kuna makabila zaidi ya 200 nchini, ambayo hutimia lugha na lahaja zaidi ya 100 (angalia orodha ya lugha hizo). Asili yao ni Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, Afrika Magharibi na Afrika Kaskazini vilevile[4].

Lugha rasmi ni Kiarabu na Kifaransa.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Table: Muslim Population by Country. Pew Research Center. Iliwekwa mnamo 16 April 2018.
  2. The World's Muslims: Unity and Diversity 128–129. Pew Forum on Religious & Public life (9 August 2012). Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-10-24. Iliwekwa mnamo 2 June 2014.
  3. Table: Christian Population as Percentages of Total Population by Country. Pew Research Center. Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-05-11. Iliwekwa mnamo 16 April 2018.
  4. Haber, Marc; Mezzavilla, Massimo; Bergström, Anders; Prado-Martinez, Javier; Hallast, Pille; Saif-Ali, Riyadh; Al-Habori, Molham; Dedoussis, George; Zeggini, Eleftheria; Blue-Smith, Jason; Wells, R. Spencer; Xue, Yali; Zalloua, Pierre A.; Tyler-Smith, Chris (1 December 2016). "Chad Genetic Diversity Reveals an African History Marked by Multiple Holocene Eurasian Migrations". The American Journal of Human Genetics (in English) 99 (6): 1316–1324. ISSN 0002-9297. PMC 5142112 Check |pmc= value (help). PMID 27889059. doi:10.1016/j.ajhg.2016.10.012. 

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Vya serikali
Vingine


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chad kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Chad Country Commercial Guide – FY 2005". Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-10-15. Iliwekwa mnamo 2021-01-16.. United States Department of Commerce.