Tibesti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Volkeno ya Emi Koussi katika safu ya Tibesti

Tibesti ni safu ya milima nchini Chadi karibu na mpaka wa Libya yenye milima mikubwa ya eneo lote la jangwa la Sahara. Asili yake ni ya kivolkeno.

Mlima mwenye kimo kikubwa ni Emi Koussi (3415 m), Kegueur Terbi (3376 m), Tarso Taro (3325 m) na Pic Tousside (3265 m) ambayo ni volkeno hai.

Sehemu za juu mlimani hupokea mvua kidogo kila mwaka kiasi hadi sentimita 12 kinachowezesha kustawi kwa mimema hata miti kadhaa. Kwa hiyo kuna wakazi wachache wa kudumu.

Zamani kabla ya kuenea kwa Sahara eneo lilikuwa na wanyamapori wengi jinsi inavyoonekana kutokana na michoro kwenye mapango iliyokuwa makazi ya kibinadamu takriban miaka 5000 iliyopita (yaani mnamo 3000 KK).


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]