N'Djamena

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ndjamena)
Jump to navigation Jump to search
Jiji la N'Djamena
Nchi Chad

Ndjamena ni mji mkuu pia mji mkubwa kabisa nchini Chad. Idadi ya wakazi hukadiriwa kuwa kati ya 800,000 na milioni moja.

Ndani ya manisipaa kuna hara au mitaa kumi.

Mtaa wa N'Djamena

Jina[hariri | hariri chanzo]

Zamani mji ulijulikana kwa jina la "Fort Lamy". Tangu 1973 jina limekuwa Ndjamena; kuna pia maandishi: N'Djaména, N'Djamena na Ndjaména.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Ndjamena uko mahali ambako mito ya Chari na Logone inaungana. Ng'ambo ya mto uko mji wa Kousseri nchini Kamerun.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ndjamena ilianzishwa na Mfaransa Émile Gentil tarehe 29 Mai 1900 kama kambi ya kijeshi ikiitwa Fort-Lamy kama kumbukumbu kwa kamanda Amédée-François Lamy aliyeuawa vitani kwenye mapigano ya Kousseri siku chache kabla ya kuanzishwa kwa Fort Lamy.

Jina lilibadilishwa kuwa Ndjamena mwaka 1973 na rais François Tombalbaye.

Mji uliona uharibifu mwingi wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe makwa 1979/1980. Wakti ule wakazi wengi waliondoka mjini lakini katika miaka ya baadaye wengi wengine waliingia.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Mji ulikua sana na haraka. Vifaa vya maji, umeme na makao havitoshi tena.

Mwaka * Idadi ya Wakazi

Makabila na vikundimjini mwaka 1993 :

 • Waarabu wa Chad : 11,08 %
 • Ngambay : 16,41 %
 • Hadjeray : 9,15 %
 • Daza : 6,97 %
 • Bilala : 5,83 %
 • Kanembou : 5,80 %
 • Maba : 4,84 %
 • Kanouri : 4,39 %
 • Gor : 3,32 %
 • Kouka : 3,20 %
 • Sar : 2,24 %
 • Barma : 2,10 %

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Ndjamena ni kitovu cha uchumi wa Chadi.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Ndjamena ina vyuo na shule mbalimbali.


Shule za Sekondari (Lycée) :

 • Lycée Félix Éboué (ya serikali)
 • Lycée technique commercial (ya seriali)
 • Lycée du Sacré-Cœur (binafsi - kikatoliki)
 • Lycée-Collège évangélique (binafsi kiprotestant)
 • Lycée Ibnou - Cinna (Kifaransa - Kiarabu)
 • Lycée Roi Faycal (Kiarabu)
 • Lycée Koweitien (Kiarabu)
 • Lycée d'Amérigue (ya serikali)
 • Lycée de Farcha (ya serikali)
 • Lycée Technique Industrielle
 • Lycée du Pont de Chagoua
 • Lycée de Waliya
 • Lycée de La Liberté
 • Lycée de la Gendarmerie, etc.

Vyuo Vikuu (Université) :

créée en 1970
 • Université Roi Fayçal (binafsi - kiislamu)

Taasisi za elimu ya juu (École Supérieure) :

 • ISSED - Institut Supérieur des Sciences de l'Éducation
 • ENAM - École Nationale d'Administration et de Magistrature
 • EIE - École Supérieure d'Électronique et d'Informatique
 • ENASS - École Nationale des Sciences Infirmières et Sociales
 • INJS - Institut Supérieur de la Jeunesse et des Sports
 • ENS - École Normale Supérieure
 • ENTP - École Nationale des Travaux Publics
 • ISTAP - Institut Supérieur des Techniques Appliquées


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]