Chari
Jump to navigation
Jump to search
Mdomo | Ziwa Chad |
Nchi | Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Kamerun |
Urefu | 1,200 km |
Kimo cha chanzo | 500 - 600 m |
Mkondo | ?? |
Eneo la beseni | 669,706 km² |
Chari (Shari) ni mto mkubwa unaoishia katika Ziwa Chad. Inaanza katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ikielekea kaskazini na kuingia nchi ya Chad. Baada ya kupita mji mkuu N'Djamena mto ni mpaka na Kamerun halafu unaishia katika Ziwa Chad.
Chari inabeba 90% ya maji yote ya kuingia ziwa Chad. Idadi kubwa ya wakazi wa nchi ya Chad wanaishi karibu na mto pamoja na mji mkuu.
Watu wanapata maisha yao mtoni kwa kilimo na uvuvi, hasa wa samaki aina ya sangara.
Tawimto muhimu ni mto Logone, mengine ni Bahr Salamat, Bahr Sarh, Bahr Aouk na Bahr Keïta.
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Chari kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |