Nenda kwa yaliyomo

Msumbiji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mozambik)
Jamhuri ya Msumbiji
República de Moçambique
Wimbo wa taifa: Pátria Amada
Mahali pa Msumbiji
Mji mkuu
na mkubwa
Maputo
Lugha rasmiKireno
Lugha ya taifaKimakhuwa, Kisena, Kitsonga, Kilomwe, Kiswahili
  Rais
Daniel Chapo
Maria Benvinda Levy
Historia
  Uhuru kutoka Ureno
25 Juni 1975
  Vita vya Kiraia vya Msumbiji
1977-1992
  Katiba ya sasa
21 Desemba 2004
Eneo
  Jumlakm2 801,590 (ya 35)
  Maji (asilimia)2.2%
Idadi ya watu
  Kadirio la 202434,881,007
  Msongamano28.7/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2023
  Jumla $53.710 bilioni
  Kwa kila mtu $1,584
PLT (Kawaida)Kadirio la 2023
  Jumla $21.936 bilioni (ya 128)
  Kwa kila mtu $647
HDI (2022) 0.461 chini
Gini (2019)Punguko chanya 50.4
SarafuMetical ya Msumbiji (MZN)
Majira ya saaUTCUTC+2 (CAT)
Upande wa magariKulia
Msimbo wa simu+258
Jina la kikoa.mz

Msumbiji ,rasmi Jamhuri ya Msumbiji ni nchi iliyoko Kusini mwa Afrika upande wa mashariki. Inapakana na Tanzania upande wa kaskazini, Malawi na Zambia kaskazini-magharibi, Zimbabwe upande wa magharibi, na Eswatini na Afrika Kusini upande wa kusini. Pia ina pwani ndefu kwenye Bahari ya Hindi upande wa mashariki. Msumbiji ina wakazi takriban milioni 33, na inashika nafasi ya 46 duniani kwa idadi kubwa ya watu. Ina eneo la takriban kilomita za mraba 801,590, na hivyo kuwa mojawapo ya nchi kubwa zaidi barani Afrika. Mji mkuu na jiji kubwa zaidi ni Maputo, ambalo ni kitovu cha kisiasa, kiuchumi, na kitamaduni cha nchi hiyo.

Msumbiji ni nchi yenye urithi wa kipekee unaochanganya tamaduni za Kiafrika na Kireno, matokeo ya karne nyingi za mwingiliano wa kihistoria. Mchanganyiko huu unaonekana katika lugha, vyakula, muziki, na mitindo ya maisha ya watu wake. Baada ya kupitia vipindi vya migogoro ya kisiasa baada ya uhuru, Msumbiji imekuwa ikijenga upya uchumi wake kupitia sekta kama kilimo, madini, nishati, na utalii wa kiikolojia. Nchi pia ina nafasi muhimu katika ushirikiano wa kikanda, ikiwa mwanachama wa mashirika kama SADC na Jumuiya ya Nchi Zinazozungumza Kireno (CPLP).

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]
Ramani ya Msumbiji

Tambarare ya pwani ni sehemu kubwa ya kusini mwa nchi, lakini kwenda kaskazini upana wake unapungua.

Nyuma ya tambarare nchi inapanda hadi kufika uwiano wa tambarare ya juu ya Afrika ya Kusini.

Milima mirefu zaidi inajulikana kama Inyanga yenye mita 2500 juu ya UB: iko katika jimbo la Tete inayopakana na Zimbabwe, Zambia na Malawi.

Mito iko mingi, mkubwa zaidi ukiwa ndio Zambezi, halafu Ruvuma mpakani kwa Tanzania, Save na Limpopo.

Ziwa la Nyassa ni sehemu ya mpaka na Malawi.

Umbo la eneo la nchi ni refu sana: ni kilomita 2000 kutoka mpaka wa Tanzania upande wa kaskazini hadi Maputo iliyoko karibu na Uswazi na Afrika Kusini.

Pwani ya Bahari Hindi ina urefu wa km 2.470.

Miji mikubwa zaidi ni Maputo (wakazi 1,080,277), Matola (wakazi 1,032,197), Nampula (wakazi 663,212) na Beira (wakazi 592,090).

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza wa Msumbiji huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne ya 4 BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi ambao walimeza wakazi wa kwanza inavyothibitishwa na DNA.

Haijulikani ni lini ya kwamba wafanyabiashara Waarabu walianza kufika ufukoni na kujenga vituo na miji yao. Lakini utamaduni wa Waswahili ulifika hadi sehemu za mwambao wa Msumbiji. Hadi leo aina ya Kiswahili inazungumzwa kwenye visiwa vya Kirimba.

Mto wa Zambezi ilitumika kama njia ya mawasiliano na biashara kati ya Ufalme wa Mwene Mtapa (Zimbabwe) na wafanyabiashara wa pwani.

Taarifa za kimaandishi zinaanza na kufika kwa Wareno. Mwaka 1498 Vasco da Gama alifika akiwa njiani kuelekea Bara Hindi.

Baadaye Msumbiji ikawa koloni la Wareno hadi mwaka 1975 vita vya ukombozi vya miaka 1964-1974 vilipomalizika kwa ushindi.

Hata hivyo vilifuata vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka 1977-1992.

Demografia

[hariri | hariri chanzo]
Mwanamke na kinyago nchini Msumbiji.

Nchini Msumbiji kuna makabila mengi sana, kama vile Wamakua, Wanyungwe, Wayao, Wamakonde na Watsonga.

Kila kabila lina lugha yake, lakini lugha rasmi ni Kireno, ambacho kinaweza kuzungumzwa na 50.3% za wakazi, ingawa ni lugha ya nyumbani kwa 16.6% tu.

Cathedral ya Beira

Upande wa dini, sensa ya mwaka 2017 ilikuta 59.2% ni Wakristo (hasa Waprotestanti na Wakatoliki, ambao ni 28.4%) na 18.9% ni Waislamu. 7.3% wanafuata dini asilia za Kiafrika au nyingine. Kumbe 13.9% hawana dini yoyote, kufuatana na kampeni ya Ukomunisti ya miaka 1979-1982.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Abrahamsson, Hans Mozambique: The Troubled Transition, from Socialist Construction to Free Market Capitalism London: Zed Books, 1995
  • Cahen, Michel Les bandits: un historien au Mozambique, Paris: Gulbenkian, 1994
  • Gengenbach, Heidi. Binding Memories: Women as Makers and Tellers of History in Magude, Mozambique. Columbia University Press, 2004. Entire Text Online
  • Mwakikagile, Godfrey, Africa and America in The Sixties: A Decade That Changed The Nation and The Destiny of A Continent, First Edition, New Africa Press, 2006, ISBN 978-0-9802534-2-9
  • Mwakikagile, Godfrey, Nyerere and Africa: End of an Era, Third Edition, New Africa Press, 2006, "Chapter Seven: "The Struggle for Mozambique: The Founding of FRELIMO in Tanzania," pp. 206–225, ISBN 978-0-9802534-1-2
  • Newitt, Malyn A History of Mozambique Indiana University Press. ISBN 1-85065-172-8
  • Pitcher, Anne Transforming Mozambique: The politics of privatisation, 1975–2000 Cambridge, 2002
  • Varia, "Religion in Mozambique", LFM: Social sciences & Missions No. 17, December 2005

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Serikali
Habari
Taarifa za jumla
Asasi zisizolenga faida
Utalii
Afya
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Msumbiji kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.