Nenda kwa yaliyomo

Matola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Matola
Nchi Tanzania
Mkoa Njombe
Wilaya Njombe Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 12,215

Matola ni kata ya Mji wa Njombe katika Mkoa wa Njombe, Tanzania, yenye postikodi namba 59118 .

Kata hiyo inaundwa na vijiji vya Matola, Mtila, Boimanda, Kitulila na Mbega.

Kijiji cha Kitulila ni kijiji muhimu zaidi cha kata hiyo kwa kuwa ndicho cha pili kwa ukubwa na kipo katikati ya barabara kuu ya Njombe kuelekea Ludewa hadi mwambao mwa ziwa Nyasa (Manda).

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 12,215 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,262 [2] walioishi humo.

Wakazi wake wengi ni Wabena (kwa asilimia zaidi ya 90), halafu Wakinga na Wapangwa.

Upande wa imani wakazi wake kwa asilimia 98 ni Wakristo wa madhehebu ya Kikatoliki, Waanglikana na Walutheri kwa idadi ndogo. Kuna makanisa rasmi matano: Kanisa Katoliki likiwa na makanisa manne na Anglikana moja, lakini pia kuna makanisa madogo yasiyo na usajili, mengi yakiwa ni madhehebu ya Kipentekoste, lakini mwitikio wake ni mdogo kiasi cha makanisa hayo kuibuka na kupotea.

Shughuli kubwa za wakazi ni kilimo cha viazi mviringo, mahindi, matunda aina ya tufaa, upandaji wa miti aina ya Pines. Upande wa mashamba kuna shamba kubwa la Chai Estate ya Dansland ambalo ni tawi la Luponde Tea Estate. Kwa hakika ardhi ni nzuri yenye rutuba na wakazi wake wengi ni watu wenye bidii.

Ndani ya kijiji hicho kuna shirika la Watawa wa Mtakatifu Agnes nyumba ya Mtakatifu Getrude Imiliwaha. Pia kuna sekondari Moja ya wasichana ya Mtakatifu Getrude inayomilikiwa na Watawa hao. Pia kuna shule za msingi mbili: Shule ya msingi Kona na Shule ya Msingi Kitulila.

Jina mbega asili yake ni mnyama mbega mwenyewe.

Kijiji cha Mbega kina sifa kedekede lakini ya kipekee ni kuwa na kundi kubwa la vijana wanaoleta chachu ya maendeleo hasa kwenye kukua kiuchumi pamoja na maendeleo ya mtu binafsi. Hivyo kimekuwa mfano kwa vijiji vingine hususan wa kujituma. Asilimia 90 ya wakazi shughuli yao kuu ni kilimo cha viazi mviringo, mahindi, maharagwe, ngano, parachichi, mbogamboga, miti ya pines pamoja na ufugaji. Kijiji hicho

Kijiji hicho kimezungukwa na mito mikubwa kama mto Mnyeleli na mto Kanyange huku kikizungukwa na milima mikubwa na midogo pamoja na misitu. Kuna mazingira mazuri na ardhi yenye rutuba inafaa kwa kuwekeza kilimo, ufugaji na hata viwanda, pamoja na miundombinu ya kudumu kama maji, umeme, shule, barabara na huduma za kiafya.

  1. https://www.nbs.go.tz, uk 209
  2. "Sensa ya 2012, Njombe - Njombe TC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-29.
Kata za Wilaya ya Njombe Mjini - Tanzania

Ihanga | Iwungilo | Kifanya | Lugenge | Luponde | Makowo | Matola | Mjimwema | Njombe Mjini | Ramadhani | Utalingoro | Uwemba | Yakobi


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Matola kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.