Nenda kwa yaliyomo

Msumbiji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Moçambique)
República de Moçambique
Jamhuri ya Msumbiji
Bendera ya Msumbiji
Lugha ya taifa Kireno
Mji Mkuu Maputo
Aina ya Serikali Jamhuri
Rais Filipe Nyusi
Waziri Mkuu Adriano Maleiane
Eneo km² 801.590
Wakazi 31,693,239 (Julai 2022)
Wakazi kwa km² 28.7
JPT/ Mkazi 233 US-$ (2004)
Uhuru kutoka Ureno tar. 25 June 1975
Pesa Metical (MZM)
Wakati UTC +2h
Wimbo wa Taifa Pátria Amada (kwa Kireno: Nchi pendwa)
Namba ya simu ya kimataifa +258
Msumbiji katika Afrika
Msumbiji katika Afrika

Msumbiji (kwa Kireno: Moçambique) ni nchi ya Afrika ya Kusini-Mashariki.

Msumbiji iko ufukoni mwa Bahari Hindi ikipakana na Tanzania, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini na Eswatini.

Upande wa mashariki kuna kisiwa cha Madagaska ng'ambo ya mlango bahari wa Msumbiji.

Jina la nchi limetokana na Kisiwa cha Msumbiji (kwa Kireno: Ilha de Moçambique) kilichokuwa boma na makao makuu ya Ureno kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki.

Sikukuu ya Taifa ni tarehe 25 Juni, ulipopatikana na uhuru mwaka 1975.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]
Ramani ya Msumbiji

Tambarare ya pwani ni sehemu kubwa ya kusini mwa nchi, lakini kwenda kaskazini upana wake unapungua.

Nyuma ya tambarare nchi inapanda hadi kufika uwiano wa tambarare ya juu ya Afrika ya Kusini.

Milima mirefu zaidi inajulikana kama Inyanga yenye mita 2500 juu ya UB: iko katika jimbo la Tete inayopakana na Zimbabwe, Zambia na Malawi.

Mito iko mingi, mkubwa zaidi ukiwa ndio Zambezi, halafu Ruvuma mpakani kwa Tanzania, Save na Limpopo.

Ziwa la Nyassa ni sehemu ya mpaka na Malawi.

Umbo la eneo la nchi ni refu sana: ni kilomita 2000 kutoka mpaka wa Tanzania upande wa kaskazini hadi Maputo iliyoko karibu na Uswazi na Afrika Kusini.

Pwani ya Bahari Hindi ina urefu wa km 2.470.

Miji mikubwa zaidi ni Maputo (wakazi 1.191.613), Matola (wakazi 543.907) na Beira (wakazi 530.706).

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza wa Msumbiji huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi ambao walimeza wakazi wa kwanza inavyothibitishwa na DNA.

Haijulikani ni lini ya kwamba wafanyabiashara Waarabu walianza kufika ufukoni na kujenga vituo na miji yao. Lakini utamaduni wa Waswahili ulifika hadi sehemu za mwambao wa Msumbiji. Hadi leo aina ya Kiswahili inazungumzwa kwenye visiwa vya Kirimba.

Mto wa Zambezi ilitumika kama njia ya mawasiliano na biashara kati ya Ufalme wa Mwene Mtapa (Zimbabwe) na wafanyabiashara wa pwani.

Taarifa za kimaandishi zinaanza na kufika kwa Wareno. Mwaka 1498 Vasco da Gama alifika akiwa njiani kuelekea Bara Hindi.

Baadaye Msumbiji ikawa koloni la Wareno hadi mwaka 1975 vita vya ukombozi vya miaka 1964-1974 vilipomalizika kwa ushindi.

Hata hivyo vilifuata vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka 1977-1992.

Mwanamke na kinyago nchini Msumbiji.

Nchini Msumbiji kuna makabila mengi sana, kama vile Wamakua, Wanyungwe, Wayao, Wamakonde na Watsonga.

Kila kabila lina lugha yake, lakini lugha rasmi ni Kireno, ambacho kinaweza kuzungumzwa na 50.3% za wakazi, ingawa ni lugha ya nyumbani kwa 16.6% tu.

Upande wa dini, sensa ya mwaka 2017 ilikuta 59.2% ni Wakristo (hasa Waprotestanti na Wakatoliki, ambao ni 28.4%) na 18.9% ni Waislamu. 7.3% wanafuata dini asilia za Kiafrika au nyingine. Kumbe 13.9% hawana dini yoyote, kufuatana na kampeni ya Ukomunisti ya miaka 1979-1982.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Abrahamsson, Hans Mozambique: The Troubled Transition, from Socialist Construction to Free Market Capitalism London: Zed Books, 1995
  • Cahen, Michel Les bandits: un historien au Mozambique, Paris: Gulbenkian, 1994
  • Gengenbach, Heidi. Binding Memories: Women as Makers and Tellers of History in Magude, Mozambique. Columbia University Press, 2004. Entire Text Online
  • Mwakikagile, Godfrey, Africa and America in The Sixties: A Decade That Changed The Nation and The Destiny of A Continent, First Edition, New Africa Press, 2006, ISBN 978-0-9802534-2-9
  • Mwakikagile, Godfrey, Nyerere and Africa: End of an Era, Third Edition, New Africa Press, 2006, "Chapter Seven: "The Struggle for Mozambique: The Founding of FRELIMO in Tanzania," pp. 206–225, ISBN 978-0-9802534-1-2
  • Newitt, Malyn A History of Mozambique Indiana University Press. ISBN 1-85065-172-8
  • Pitcher, Anne Transforming Mozambique: The politics of privatisation, 1975–2000 Cambridge, 2002
  • Varia, "Religion in Mozambique", LFM: Social sciences & Missions No. 17, December 2005

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Serikali
Habari
Taarifa za jumla
Asasi zisizolenga faida
Utalii
Afya


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Msumbiji kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.