Afrika Kusini : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Badiliko: wa:Nonne-Afrike
Mstari 353: Mstari 353:
[[ny:South Africa]]
[[ny:South Africa]]
[[oc:Sud-Africa]]
[[oc:Sud-Africa]]
[[or:ଦକ୍ଷିଣ ଆଫ୍ରିକା]]
[[os:Хуссар Африкæйы Республикæ]]
[[os:Хуссар Африкæйы Республикæ]]
[[pa:ਸਾਊਥ ਅਫ਼ਰੀਕਾ]]
[[pa:ਸਾਊਥ ਅਫ਼ਰੀਕਾ]]

Pitio la 18:28, 3 Februari 2012

Afrika Kusini


Afrika Kusini ni nchi kubwa ya Afrika ya Kusini yenye wakazi takriban milioni 45. Imepakana na Namibia, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji na Uswazi. Nchi ya Lesotho iko ndani ya eneo la Afrika Kusini.

Mji mkubwa ni Johannesburg. Wajibu wa mji mkuu yamegawiwa kwa mji mitatu: Cape Town ni makao ya Bunge, Pretoria ni makao ya Serikali na Bloemfontein ni makao ya Mahakama Kuu.

Nchi ina majina rasmi 11 kutokana na lugha rasmi 11. Ndizo Kiafrikaans, Kiingereza, Kizulu, Kixhosa, Kiswati, Kindebele, Kisotho cha Kusini, Kisotho cha Kaskazini, Kitsonga, Kitswana, Kivenda.

Kati ya watu mashuhuri sana wa Afrika Kusini ni Nelson Mandela aliyekuwa rais kati ya 1994 hadi 1999. Wengine ni Christiaan Barnard (daktari wa kwanza duniani aliyehamisha moyo wa mtu kwa mtu mwingine) na Shaka Zulu aliyekuwa kiongozi wa kijeshi kabla ya ukoloni.

Historia

Koloni ya Waholanzi kwenye Rasi

Chanzo cha Afrika Kusini kama nchi ni Koloni ya Rasi iliyoundwa na Waholanzi katika eneo la Cape Town. Hapa kabila jipya la Makaburu lilijitokeza kati ya walowezi Wazungu kutoka Uholanzi, Ufaransa na Ujerumani; lugha yao ilikuwa Kiholanzi iliyoanza kuchukua maneno ya Kifaransa, Kiafrika na Kiingereza na kuendelea kuwa lugha ya pekee Kiafrikaans.

Karne za kwanza za koloni ya Kiholanzi ziliona pia kufika kwa watumwa kutoka Indonesia walioletwa hapa kama wafanyakazi kwa Waholanzi na Makaburu. Hao Waindonesia walikuwa chano cha jumuiya ya Kiislamu kwenye rasi. Pia chotara walitokea kutokana na kuzaa kati ya Makaburu na wanawake Waafrika na Waindonesia. Sehemu ya chotara hao wameingia katika jumuiya ya makaburu na wengi wao wanapimwa kuwa na mababu Waaafrika. Katika miaka ya baadaye ubaguzi wa rangi uliongezeka na watoto wa wazungu na Waafrika au chotara mara nyingi hawakukubaliwa walianza kuishi kama kundi la pekee kati ya Waafrika na Wazungu ni chanzo cha hao walioitwa baadaye "Cape Coloreds".

Milki za Waafrika na Mfecane

Sehemu kubwa kaskazini za rasi zilikaliwa na makabila ya Waafrika. Mnamo mwaka 1800 falme na milki zilianza kutokea hapa. Mwanzo wa karne ya 19 ni hasa Wazulu chini ya Shaka Zulu walioanza kuenea na kuwashambulia majirani katika vita za mfecane. Vita hizi zilileta uharibifu mkubwa lakini zilisababisha pia kutoeka kwa milki za Wasotho na Watswana na wengine walioiga mitindo ya Wazulu na kujenga madola yenye wezo wa Kijeshi.

Kuingia kwa Uingereza na jamhuri za Makaburu

Mwaka 1814 Koloni ya Rasi ilitwaliwa na Waingereza na kuwa sehemu ya Milki ya Uingereza. Makaburu hao walihama kwenda kaskazini wakaanzisha jamhuri ndogo kati ya maeneo ya Waafrika ama kwa njia ya mapatano nau au kwa njia ya kivita.

Utawala wa Kiingereza ulisababisho uhamisho wa nje wa sehemu ya Makaburu waliotokana na Wazungu kutoka Uholanzi, Ufaransa na Ujerumani; Makaburu hao walihama kwenda kaskazini wakaanzisha jamhuri ndogo kati ya maeneo ya Waafrika ama kwa njia ya mapatano nau au kwa njia ya kivita.

Kati ya 1840 na 1850 Waingereza waliwafuata Makaburu kwa kueneza maeneo yao hadi mto Oranje; walikamata jamhuri ya Kimakaburu ya Natalia na kuanzisha koloni mpya ya Natal.

Jamhuri mbili za Makaburu ziliweza kustawi kwa miaka kadhaa ambazo zilikuwa jamhuri ya Dola Huru la Oranje upande wa kaskazini ya mto Oranje na jamhuri ya Transvaal (ilijiita pia Jamhuri ya Kiafrika ya Kusini) upande wa kaskazini ya mto Vaal.

Waafrika, Waingereza na Makaburu waligongana

Milki za Kiafrika zilitafuta njia zao kati ya himaya hizi za Wazungu ambao waliokuwa na nguvu kutokana na silaha za kisasa. Wengine walitafuta uhusiano mzuri na Makaburu na kushikamana nao; wengine waliona Makaburu kama hatari wakatafuta uhusiano wa ulinzi na Waingereza. Mikataba kati ya Waingereza na milki za Kiafrika iliunda nchi lindwa zinazoendelea hadi leo kama nchi huru kama vile Botswana (Bechuanaland), Lesotho na Uswazi (Swaziland).

Katika miaka ya 1880 almasi na dhahabu zilipatikana kwa wingi katika jamhuri hizi na kusababisha kufika kwa wachimba madini wengi, hasa Waingereza, waliotaka kutajirika; Makaburu walisita kuwapa haki za kiraia kwa sababu waliogopa wageni wengi. Tatizo hili lilisababisha vita ya Makaburu didi ya Uingereza na jamhuri za Makaburu zilitwaliwa na jeshi la Kiingereza hadi mwaka 1902 zikawa koloni.

Karne ya 20: Muungano wa Afrika Kusini

Jitihada za kupatanisha Wazungu wa Afrika Kusini yaani Waingereza na Makaburu zilileta kuundwa kwa Muungano wa Afrika Kusini kama nchi ya kujitawala ndani ya Milki ya Uingereza. Waafrika kwa jumla hawakuwa na haki za kiraia katika nchi hii isipokuwa katika Jimbo la Rasi kama walikuwa na mapato ya kulipa kodi za kutosha na elimu.

Siasa ya Apartheid tangu 1948

Baada ya vita kuu ya pili ya dunia chama cha National kilichofuata itikadi kali ilipata kura nyingi na kuchukua serikali ya Afrika Kusini. Ilianzisha mfumo wa ubaguzi wa rangi kwa jina la apartheid. Haki za wasio Waungu zilipungukiwa zaidi. Maeneo ya Kiafrika yalitangazwa kuwa nchi za pekee chini ya usimamizi wa serikali ya kizungu ya Afrika Kusini; kwa hiyo wananchi kutoka meneo haya hawakuwa tena na haki za kuchukua rufaa mbele ya mahakama walipewa vibali vya muda tu kukaa kwenye miji. Waafrika walipaswa kutemeba muda wote na pasipoti na vibali; ndoa na mapenzi kati ya watu wa rangi mablimbali zilipigwa marufuku. Shule na makazi zilitenganishwa.

Siasa hii ilisababisha faakano kati ya nchi nyini za dunia na Afrika Kusini. Upinzani kutoka Uingereza na Jumuiya ya Madola ulisababisha kuondoka kwa Afrika ya Kusini katika jumuiya hii na kutangazwa kwa Jamhuri ya Afrika Kusini.

Afrika Kusini mpya

1990 Apartheid ilikwisha na serikali ya National Party ilipaswa kuendesha uchaguzi huru kwa wananchi wote na kukabidhi madaraka kwa serikali ya ANC chini ya Nelson Mandela.

Uchumi

Kiuchumi Afrika Kusini ni nchi yenye pande mbili kabisa. Sehemu ya uchumi ina hali ya kimaendeleo kabisa ikiwa viwanda na huduma za Afrika Kusini zinalingana na hali ya juu kabisa duniani na hali ya maisha ya wananchi waliomo katika sekta hii inalingana na nchi kama Australia au Ulaya ya magharibi. Kwa upande mwingine hali ya maisha ya sehemu kubwa ya wananchi ni umaskini kama katika sehemu nyingine za Afrika au Uhindi wa mashambani. Lakini kwa ujumla hali ya maisha iko juu kuliko nchi nyingi za Afrika.

Sekta muhimu za uchumi ni migodi ya kuchimba dhahabu au almasi, viwanda na huduma kama benki au bima.


Utawala na muundo wa shirikisho

Afrika Kusini ni shirikisho. Katiba mpya ya 1997 iliendeleza muundo huu uliundwa kama "Umoja wa Afrika Kusini" baada ya vita ya makaburu dhidi Uingereza. Afria ya Kusini ya kale ilikuwa na majimbo manne ya (Rasi, Natal, Dola Huru la Mto Orange na Transvaal). Maeneno makubwa yaliyokaliwa na Waafrika yalibaki nje katika katiba ya Apartheid yakiitwa bantustan (au: homeland). Katiba mpya ilichora mipaka upya.

Majimbo ya Afrika Kusini

Ramani ya majimbo na wilaya za Afrika Kusini

Mji mkuu wa jimbo watajwa katika mabano.

  1. Rasi ya Magharibi (Western Cape)¹ (Cape Town) kifupi: WC
  2. Rasi ya Kaskazini (Northern Cape) (Kimberley) kifupi: NC
  3. Rasi ya Mashariki (Eastern Cape) (Bhisho) kifupi: EC
  4. KwaZulu-Natal (Pietermaritzburg²) kifupi: KZ, KZN or KN
  5. Dola Huru (Free State) (Bloemfontein) kifupi: FS
  6. Kaskazini-Magharibi (Mafikeng) kifupi: NW
  7. Gauteng (Johannesburg) kifupi: GT or GP
  8. Mpumalanga (Nelspruit) kifupi: MP
  9. Limpopo (Polokwane) kifupi: LP

Miji Mikubwa

Ramani ya Afrika Kusini

Hii ni miji/ manisipaa/ jiji kumi yenye wakazi wengi nchini.

Na. Munisipaa au Jiji Wakazi (2001) Wakazi (1996) Asilimia ya badiliko
1996-2001
1. Johannesburg, Gauteng 3,225,812 2,639,110 22.2%
2. Durban, KwaZulu-Natal 3,090,117 2,751,193 12.3%
3. Cape Town, Rasi ya Magharibi 2,893,251 2,563,612 12.9%
4. East Rand, Gauteng 2,480,282 2,026,807 22.4%
5. Pretoria, Gauteng 1,985,984 1,682,701 18.0%
6. Port Elizabeth, Rasi ya Mashariki 1,005,776 969,771 3.7%
7. East London, Rasi ya Mashariki 701,881 682,287 2.9%
8. Vereeniging, Gauteng 658,422 597,948 10.1%
9. Bloemfontein, Dola Huru 645,441 603,704 6.9%
10. Thohoyandou, Limpopo 584,469 537,454 8.7%

Jeshi

Jeshi la Afrika Kusini ina silaha za kisasa kushinda nchi zote za majirani. Uchumi unawezesha nchi ya kutumia kiasi kikubwa kwa ajili ya jeshi kuliko nchi zote za Afrika kusini ya Sahara.

Afrika Kusini iliwahi kuwa na silaha za kinyuklia lakini ilizibomoa baada ya mwaka 1993.

Angalia pia

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Afrika Kusini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.



Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA