Christiaan Barnard

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Christiaan Barnard (1968)

Christiaan Neethling Barnard (8 Novemba 19222 Septemba 2001) alikuwa daktari mpasuaji nchini Afrika Kusini. Barnard ni maarufu kwa sababu alikuwa daktari wa kwanza aliyehamisha moyo wa mtu kwa mtu mwingine.

Christian alizaliwa katika familia maskini ya mhubiri makaburu. Akasoma tiba kwenye chuo kikuu cha Cape Town na baadaye huko Marekani kwenye chuo kikuu cha Minnesota alipoendelea kupata diploma ya upasuaji.

1958 alirudi Afrika Kusini akawa bingwa wa upasuaji wa moyo na profesa kwenye chuo kikuu.

Uhamisho wa moyo[hariri | hariri chanzo]

Tar. 3 Desemba 1967 katika hospitali ya Groote Schuur mjini Cape Town Christiaan Barnard alikuwa daktari kiongozi katika upasuaji uliofaulu mara ya kwanza kuhamisha moyo kutoka kwa mtu kwenda mtu mwingine. Jumla ya madaktari 31 walishirikiana kumpatia mgonjwa Louis Washkansky mwenye miaka 54 moyo wa kijana Denise Darvall aliyewahi kufa siku ileile hospitalini kutokana na ajali ya motokaa akiwa na umri wa miaka 25.

Upasuaji uliendelea kwa masaa matano. Washkansky aliishi siku 18 na moyo mpya akafa baadaye kutokana na uambukizo wa mapafu.

Mgonjwa wa pili aliyepokea moyo mpya na Barnard alikuwa Philip Blaiberg tar. 2 Januari 1968 akaendelea kuishi miezi 19.

Barnard alianzisha mbinu huu ulioendelezwa baadaye. Siku hizi takriban theluthi mbili ya watu waliopokea moyo mpya huishi zaidi ya miaka mitano.