Cabo Verde
Jamhuri ya Cabo Verde | |
---|---|
República de Cabo Verde (Kireno) | |
Kaulimbiu ya taifa: Unidade, Trabalho, Progresso (Kireno) "Umoja, Kazi, Maendeleo" | |
Wimbo wa taifa: Cântico da Liberdade (Kireno) "Mkarara wa Uhuru" | |
Mahali pa Cabo Verde | |
Ramani ya Cabo Verde | |
Mji mkuu na mkubwa nchini | Praia |
Lugha rasmi | Kireno Kikaboverde |
Serikali | Jamhuri |
• Rais • Waziri Mkuu | José Maria Neves Ulisses Correia e Silva |
Eneo | |
• Eneo la jumla | km2 4 033[1] |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 603 901[1] |
Pato la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 2.598[2] |
• Kwa kila mtu | USD 4 503[2] |
Pato halisi la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 5.717[2] |
• Kwa kila mtu | USD 9 909[2] |
Maendeleo (2021) | 0.662[3] - wastani |
Sarafu | Escudo ya Cabo Verde |
Cabo Verde (Kiingereza: Cape Verde) ni nchi ya visiwa katika bahari ya Atlantiki mbele ya pwani ya Afrika ya Magharibi.
Umbali wake na Senegal ni km 460.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Eneo la visiwa vyake kwa jumla ni km² 4,033.
Funguvisiwa lake lina visiwa 15 katika vikundi viwili:
- Visiwa "juu ya upepo" (Barlavento): Santo Antão, São Vicente, São Nicolau, Sal, Boa Vista na visiwa bila watu vya Santa Luzia, Branco na Razo.
- Visiwa "chini ya upepo" (Sotavento): Maio, Santiago, Fogo, Brava na visiwa bila watu vya Ilheus Secos ou do Rombo.
Miji
[hariri | hariri chanzo]Mji mkuu ni Praia katika kisiwa cha Santiago.
Miji mikubwa zaidi ni (takwimu za mwaka 2010): Praia (wakazi 127,832), Mindelo (wakazi 70,468), Santa Maria (wakazi 23,839), Assomada (wakazi 12,026), Pedra Badejo (wakazi 9,345) na São Filipe (wakazi 8,125).
Historia
[hariri | hariri chanzo]Hadi kufika kwa Wareno katika karne ya 15 visiwa vya Cabo Verde havikuwa na watu.
Wareno walianzisha mashamba ya miwa na kuleta watumwa kutoka bara la Afrika.
Cabo Verde ilikuwa pia kituo muhimu cha biashara ya watumwa kati ya Afrika na Amerika.
Wahamiaji kutoka Ulaya walikuwa pia Wahispania, Waitalia pamoja na Wayahudi na Waislamu waliokataliwa kukaa kwao Ureno.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Kutokana na historia hiyo, leo idadi kubwa ya wakazi ni machotara waliozaliwa na Waafrika (waliochangia 56% ya DNA) na Wazungu (waliochangia 44%).
Lugha rasmi ni Kireno, lakini wakazi wanazungumza zaidi aina mbalimbali za Krioli iliyotokana na lugha hiyo.
Upande wa dini, walau 89.1% ya wakazi ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (78.7%), lakini pia wa madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (10.4%).
Kutokana na hali ngumu ya uchumi, wananchi wanaoishi nje ya Cabo Verde ni mara mbili kuliko wale wanaoishi nchini. Kati ya waliohama baada ya uhuru (1975), 500,000 wanaishi Marekani na 150,000 Ureno. Hata hivyo kuna wahamiaji vilevile, hasa kutoka nchi za Afrika bara.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Cabo Verde". The World Factbook (kwa Kiingereza) (tol. la 2024). Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo 23 Machi 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 "World Economic Outlook Database, October 2023 Edition. (Cape Verde)". IMF.org. International Monetary Fund. 26 Machi 2024. Iliwekwa mnamo 26 Machi 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Human Development Report 2020 The Next Frontier: Human Development and the Anthropocene (PDF). United Nations Development Programme. 15 Desemba 2020. ku. 343–346. ISBN 978-92-1-126442-5. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 15 Desemba 2020. Iliwekwa mnamo 16 Desemba 2020.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
- J.Pim, C. Pierce, A.B.Watts, I. Grevemeyer, A. Krabbenhoeft (5 Mei 2008). "Crustal structure and origin of the Cape Verde Rise" (PDF). Earth and Planetary Science Letters. 272. Elesiever: 422–428. doi:10.1016/j.epsl.2008.05.012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2011-01-06. Iliwekwa mnamo 2015-07-18.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) - Carling, Jorgen (2004). "Emigration, Return and Development in Cape Verde: The Impact of Closing Borders". Population, Space and Place. 55 (10). John Wiley & Sons, Ltd.: 113–132. doi:10.1002/(SICI)1097-4679(199901)55:1<117::AID-JCLP12>3.0.CO;2-A. PMID 10100838.
- Ramalho, R.; Helffrich, G.; Schmidt, D.; Vance, D. (2010). "Tracers of Uplift and Subsidence in the Cape Verde Archipelago". Journal of the Geological Society. 167 (3). London: Geological Society of London: 519–538. doi:10.1144/0016-76492009-056.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Official website of the Government of Cape Verde
- Cabo Verde katika Open Directory Project
- Cape Verde entry at The World Factbook
- Cape Verde from State.gov
- Country Profile from BBC News
- Cape Verde entry on Encyclopædia Britannica
- Cape Verde Ilihifadhiwa 7 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Key Development Forecasts for Cape Verde from International Futures
- Cape Verde 2012
- Amateur Radio Cabo Verde
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Cabo Verde kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |