Ujerumani
|
|||||
| Wito la taifa: Einigkeit und Recht und Freiheit (Kijerumani: "Umoja na Haki na Uhuru”) |
|||||
| Wimbo wa taifa: Wimbo wa Wajerumani (beti ya tatu) Umoja na Haki na Uhuru |
|||||
| Mji mkuu | Berlin |
||||
| Mji mkubwa nchini | Berlin | ||||
| Lugha rasmi | Kijerumani 1 | ||||
| Serikali | Shirikisho la Jamhuri Joachim Gauck Angela Merkel |
||||
| Dola Takatifu la Kiroma Dola la Ujerumani Shirikisho la Jamhuri Maungano |
843 (Mkataba wa Verdun) 18 Januari 1871 23 Mei 1949 3 Oktoba 1990 |
||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
357,050 km² (ya 63) 2.416 |
||||
| Idadi ya watu - 2005 kadirio - 2000 sensa - Msongamano wa watu |
82,438,000 (ya 14) N/A 230.9/km² (ya 50) |
||||
| Fedha | Euro (€) 2 (EUR) |
||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
| Intaneti TLD | .de | ||||
| Kodi ya simu | +49 |
||||
| 1 Kideni, Kijerumani cha Kaskazini, Kisorbia, Kifrisia ni lugha rasmi katika mikoa kadhaa 2 hadi 1999: Mark (DM) | |||||
Ujerumani, Kijerumani: Deutschland (pia: Udachi) ni nchi ya Ulaya ya Kati. Imepakana na Denmark, Poland, Ucheki, Austria, Uswisi, Ufaransa, Luxemburg, Ubelgiji na Uholanzi.
Ni nchi yenye watu wengi katika Ulaya isipokuwa Urusi ina watu zaidi. Uchumi wa Ujerumani una uwezo mkubwa ni nchi inayouza bidhaa nyingi nje kushinda mataifa yote ya dunia.
Muundo wake ni shirikisho la jamhuri lenye majimbo 16 ndani yake na kila jimbo lina kiwango cha kujitawala.
Lugha asilia ya wenyeji ni Kijerumani kinachojadiliwa kwa lahaja mbalimbali lakini wenyeji wote wanasikilizana. Katika maeneo mawili kuna wasemaji asilia wa Kideni na Kisorbia. Wahamiaji wa karne ya 20 wameleta lugha zao wasa Kituruki na lugha za Ulaya ya Kusini.
Yaliyomo |
Jina la Nchi [hariri]
Wenyeji wanaiita "Deutschland" (
Deutschland (info), tamka: doich-land) na jina hili limeingia katika Kiswahili kama "Udachi". Lilikuwa jina la kawaida katika karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20. Siku hizi neno "Ujerumani" limechukua nafasi yake linalotokana na Kiingereza "Germany".
Jiografia [hariri]
Ujerumani inaenea kati ya bahari upande wa kaskazini na milima ya Alpi upande wa kusini. Mipaka yake upande wa magharibi na mashariki ilibadilika mara nyingi katika historia yake; tangu 1945 mpaka wa madhariki ni mto Oder. Upande wa magharibi sehemu ya mpaka ni mto Rhein.
Kuna kanda tatu za kijiografia:
- tambarare ya pwani ya kaskazini
- kanda ya vilima
- milima ya kusini pamoja na Alpi.
Tambarare ya pwani ya kaskazini ni eneo bapa; hakuna milima yenyewe na nchi haipandi juu ya mita 200, sehemu kubwa ni kati ya uwiano wa bahari na mita 60 juu yake.
Historia [hariri]
- Dola Takatifu la Kiroma (900-1806)
- Shirikisho la Ujerumani (1815-1866)
- Dola la Ujerumani (1871-1945)
- Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani (1949 hadi 1990 Ujerumani wa Magharibi)
- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani (1949 hadi 1990 Ujerumani wa Mashariki)
Miji [hariri]
Majiji yenye wakazi zaidi ya milioni moja ni
Miji mikubwa mingine ni
Majimbo [hariri]
Baden-Württemberg
Bavaria (Freistaat Bayern)
Berlin
Brandenburg
Bremen (Freie Hansestadt Bremen)
Hamburg (Freie und Hansestadt Hamburg)
Hesse (Hessen)
Mecklenburg-Pomerini (Mecklenburg-Vorpommern)
Saksonia Chini (Niedersachsen)
Rhine Kaskazini-Westfalia (Nordrhein-Westfalen)
Rhine-Palatino (Rheinland-Pfalz)
Jimbo la Saar (Saarland)
Saksonia (Freistaat Sachsen)
Saksonia-Anhalt (Sachsen-Anhalt)
Schleswig-Holstein
Thuringia (Freistaat Thüringen)
Waja [hariri]
- Michael Ballack
- Ludwig van Beethoven
- Papa Benedikto XVI
- Johannes Brahms
- Johann Wolfgang von Goethe
- Günter Grass
- Johannes Gutenberg
- Immanuel Kant
- Martin Luther
- Friedrich Nietzsche
- Valentin Weigel
| Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ujerumani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
|
||||||||||||||