Mchanga
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchanga ni punje ndogo za mwamba uliosagwa.
Kufuatana na mapatano ya kitaalamu mawe huitwa "mchanga" kama punje zake ziko kati ya milimita 0.063 hadi 2.
Punje hizi zatokana na mmomonyoko wa mawe makubwa zaidi kama changarawe yaliyosukumwa na upepo au maji kwa mfano mtoni, baharini au kwenye mtelemko wa mlima.
Mchanga hupatikana kwa wingi hasa kando la bahari, jangwani au mtoni.
Mchanga ukichanganywa na saruji na maji huwa zege inayotumiwa kwa ujenzi.
-
Njia ya mchanga Namibia
| Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mchanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |