Hadubini
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hadubini (pia: darubini ya vidudu) ni kifaa cha kutazama vitu vidogo sana. Ni chombo muhimu cha sayansi kwa utafiti wa vitu ambavyo ni vidogo mno kwa jicho la kibinadamu.
Hadubini ya kawaida (hadubini maonzi) huwa na lenzi zinazokuza kiolwa kinachowekwa chini yake. Kwa kawaida kuna lenzi kadhaa zenye viwango tofauti vya kukuza. Muundo wake hufanana na darubini lakini inaangalia vitu kwa karibu ambavyo ni vidogo kimaumbile. Darubini inaangalia violwa vya mbali vinayoonekana vidogo kutokana na umbali.
Uwezo wa hadubini ya kawaida ni kukuza hadi mara 1,500.
Kwa utafiti wa vitu vidogo zaidi kuna teknolojia ya hadubini elektronia. Kifaa hiki hutumia elektroni badala ya nuru kwa utafiti wake na kuwezesha kutazama yaliyomo ya molekuli.
[hariri] Viungo vya Nje
[hariri] Tazama pia
| Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hadubini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |

