Miwani
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama hapa
Mtu mwenye miwani (Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania)
Miwani ni msaada wa kuona vizuri zaidi kinachotumiwa na watu wenye macho madhaifu. Ni kifaa kinachoboresha uwezo wa kuona.
Kwa kawaida miwani ni lenzi mbili za kioo au plastiki zinazoshikwa na fremu. Fremu hulala juu ya pua ikiwa na mikono miwili inayoshikana na masikio.
Aina za lenzi zinateuliwa kutokana na udhaifu wa macho yaani tabia ya lenzi inapaswa kulingana na tatizo la kila jicho.
Kuna pia miwani ya kukinga macho ama dhidi ya jua kali au dhidi ya upepo na vumbi wakati wa kufanya kazi au kwenye burudani ya michezo.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
| Makala hiyo kuhusu "Miwani" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Miwani kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |