Köln

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Köln






Köln

Bendera

Nembo
Köln is located in Ujerumani
Köln
Köln

Mahali pa mji wa Köln katika Ujerumani

Majiranukta: 50°56′0″N 6°57′0″E / 50.93333°N 6.95000°E / 50.93333; 6.95000
Nchi Ujerumani
Jimbo Rhine Kaskazini - Westfalia
Idadi ya wakazi (2019)
 - Wakazi kwa ujumla 1.087.863
Tovuti:  www.koeln.de

Köln (pia: Kolon, kutokana na Kiingereza Cologne; kwa Kijerumani cha kienyeji: Kölle) ni mji wa Ujerumani kando ya mto Rhine wenye wakazi 970,000.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Maana asili ya jina ni "koloni". Ni mji wa kale ulioundwa kwa jina la "Colonia Claudia Ara Agrippinensis" kama koloni ya Waroma wa Kale mnamo mwaka 50. Mahali pa mji paliwahi kuwa boma la Kiroma na kabla ya hapo kijiji cha kabila cha Waubii.

Köln ni mji mkubwa wa nne wa Ujerumani na mji mkubwa wa jimbo la Rhine Kaskazini - Westfalia (Nordrhein-Westfalen).

Kuna kanisa kubwa kuliko yote ya Ujerumani ("Kölner Dom") ambalo ni maarufu kwa sababu limejengwa katika muda wa miaka 700 tangu mwaka 1248 hadi 1880. Masalia ya mamajusi watatu waliomtembelea mtoto Yesu huko Bethlehemu yanasemekana kutunzwa humo. Köln ni kitovu muhimu wa Kanisa Katoliki nchini na makao wa askofu mkuu.

Chuo kikuu chake kilianzishwa mwaka 1388 na leo kuna wanafunzi 44,000 na pamoja na vyuo vingine kuna wanafunzi zaidi ya 80,000 kwenye ngazi ya vyuo. Kati ya vyuo vingine Chuo cha Muziki kimejulikana sana kimataifa.

Mji umejulikana pia kwa aina yake ya pekee ya bia.

Köln ni pia kitovu cha Waafrika katika Ujerumani. Pamoja na wanafunzi wengi kutoka Afrika kuna pia taasisi kama huduma ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) zinazoajiri Waafrika wengi. Kuna hata vilabu ambako bia aina ya Tusker kutoka Kenya inauzwa.

Mwaka 2005 Köln ilikuwa mahali pa Siku ya kimataifa ya vijana Wakatoliki; zaidi ya milioni moja walikutana na Papa Benedikto XVI.

Watalii wengi wanafika kila mwaka kwa sherehe ya Karnivali kabla ya majira ya Kwaresima.

Picha[hariri | hariri chanzo]


Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Köln kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.