Yosefu (mume wa Maria)
Yosefu (kwa Kiebrania יוֹסֵף, "Yosef"; kwa Kigiriki Ἰωσήφ), kadiri ya Injili, alikuwa mume wa Bikira Maria na baba mlishi wa Yesu Kristo ambao pamoja naye waliunda Familia takatifu.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Injili ya Mathayo (13:5) inamsifu kwa uadilifu wake na kumtaja kama "fundi" (kwa Kigiriki téktón). Lakini inasema pia (sawa na Injili ya Luka) kuwa alitoka katika ukoo wa mfalme Daudi. Ndiye aliyetunza familia hiyo kwa kazi ya mikono yake na kumfundisha mtoto Yesu kufanya kazi za kibinadamu.
Injili na imani ya Kikristo zinasisitiza kuwa baba halisi wa Yesu alikuwa Mungu mwenyewe: Maria alimchukua mimba kwa muujiza uliosababishwa na Roho Mtakatifu.
Yosefu, kisha kujulishwa juu ya mimba hiyo, alikubali kumchukua mchumba wake nyumbani na kumtambua mwanae kuwa ni wa kwake ingawa hakuwahi kujamiiana naye. Hivyo alitunza heshima ya mama na mtoto na kuwahakikishia ulinzi katika jamii inayojali zaidi wanaume.
Miezi baadaye yeye na Maria walikwenda Bethlehemu kwa ajili ya sensa, na ndipo Yesu alipozaliwa pangoni na kulazwa horini.
Wakati huo Yosefu alishuhudia ujio wa wachungaji waliokuja kumuabudu mtoto kadiri ya tangazo la malaika waliowatokea.
Kadiri ya Torati ya Musa, siku nane baada ya mtoto kuzaliwa, Yosefu alimpa mtoto jina wakati wa kutahiriwa, na siku arubaini baadaye alimpeleka hekaluni Yerusalemu ili kumtolea Mungu kama mtoto wa kiume wa kwanza. Ndipo wazee Simeoni na Anna binti Fanueli walipotoa utabiri juu ya Yesu.
Baada ya mamajusi kuwatembelea Bethehemu, wanafamilia walikimbilia Misri ili kukwepa dhuluma ya mfalme Herode Mkuu aliyetaka kumuua mtoto kwa kuogopa atampindua baadaye.
Kisha wakarudi Nazareti (Galilaya) ambapo Yesu alikua vizuri chini ya wazee wake.
Yesu alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote watatu walikwenda kuhiji Yerusalemu kwa Pasaka. Wakati wa kurudi, mtoto alibaki mjini akapatikana tena siku ya tatu akiwa hekaluni kati ya walimu wa sheria, akitokeza hekima yake. Alipoulizwa na Maria kuhusu mwenendo wake, mtoto alionyesha kujitambua si mwana wa Yosefu, bali wa Mungu. Hata hivyo alizidi kumheshimu na kumtii yeye kama baba pamoja na Mama Maria.
Baada ya taarifa hiyo, hakuna tena habari juu ya Yosefu, hivi kwamba wengi wanajiuliza kuhusu kifo chake na kuhisi kilikuwa kimeshatukia Yesu alipoanza utume wake.
Heshima baada ya kifo
[hariri | hariri chanzo]Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Heshima hiyo ilizidi kukua hasa magharibi kadiri ulivyozingatiwa ubinadamu wa Yesu.
Hatimaye alitangazwa na Mapapa kuwa msimamizi wa Kanisa lote kwa jinsi alivyosimamizi vizuri familia takatifu na katika karne ya 20 na ya 21 jina lake limeingizwa katika sala za ekaristi zote za liturujia ya Roma.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Machi, mbali ya kumbukumbu yake kama mfanyakazi tarehe 1 Mei iliyoongezwa na Papa Pius XII mwaka 1955 ili kuwapa kielelezo na msimamizi wafanyakazi Wakristo wanaosherehekea siku hiyo pamoja na wenzao wa sehemu nyingi za dunia Sikukuu ya kazi [1].
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Ndoto ya Yosefu, kadiri ya Rembrandt, 1645 hivi
-
Ndoa na Bikira, kadiri ya Perugino, 1448 hivi
-
Kuzaliwa kwa Yesu, kadiri ya Marten de Vos 1577
-
Ibada ya Mamajusi, kadiri ya Hans Memling, 1480 hivi
-
Yesu kutolewa hekaluni, kadiri ya di Fredi, 1388
-
Ndoto ya kukimbilia Misri, kadiri ya Daniele Crespi, 1625 hivi
-
Kukimbilia Misri, kadiri ya Giotto, karne ya 14
-
Kupatikana hekaluni, Breviari ya karne ya 15
-
Kifo cha Yosefu, St. Martin's at Florac
-
Yosefu kutiwa taji, Valdés Leal, 1670 hivi
Katika muziki
[hariri | hariri chanzo]- Nicolas Chadeville (1696 - 176?): Joseph est bien Marié, a choral composition (1755)
- The Killers: Joseph, Better You Than Me (2007)
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- verett Ferguson, Michael P. McHugh, Frederick W. Norris, "Encyclopedia of early Christianity, Volume 1", article Joseph, p.629
- Crossan, John Dominic. Jesus : A Revolutionary Biography. Harpercollins: 1994. ISBN 0-06-061661-X.
- Dickson, John. Jesus: A Short Life, Lion Hudson plc, 2008, ISBN 0-8254-7802-2, ISBN 978-0-8254-7802-4, Google Books
- Fiensy, David A.; Jesus the Galilean: soundings in a first century life, Gorgias Press LLC, 2007, ISBN 1-59333-313-7, ISBN 978-1-59333-313-3, Google books Ilihifadhiwa 11 Mei 2015 kwenye Wayback Machine.
- Catholic Encyclopedia article
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Joseph. (2010). In Encyclopædia Britannica. Retrieved 7 Mei 2010, from Encyclopædia Britannica Online
- The Life of St. Joseph, Spouse of the Blessed Virgin Mary and foster-father of Our Lord Jesus Christ Ilihifadhiwa 20 Agosti 2014 kwenye Wayback Machine.
- Saint Joseph Ilihifadhiwa 1 Machi 2014 kwenye Wayback Machine. at Patron Saints Index
- Catholic Online Saints: St. Joseph* Eastern Orthodox Tradition: The Righteous Elder Joseph The Betrothed, And His Repose Archived 2013-01-13 at Archive.today
- Holy Righteous Joseph the Betrothed Orthodox icon and synaxarion for the Sunday after Nativity
- Translation of Grimm's Legend No. 1 Saint Joseph in the Forest Ilihifadhiwa 6 Desemba 2016 kwenye Wayback Machine.
- The vocation of Saint Joseph Ilihifadhiwa 26 Oktoba 2013 kwenye Wayback Machine. at Early Christians
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yosefu (mume wa Maria) kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |