Nenda kwa yaliyomo

Sao Tome na Principe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka São Tomé and Príncipe)
República Democrática de São Tomé e Príncipe
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Sao Tome na Principe
Bendera ya Sao Tome na Principe Nembo ya Sao Tome na Principe
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: n/a
Wimbo wa taifa: Independência total (Uhuru Kamili)
Lokeshen ya Sao Tome na Principe
Mji mkuu Sao Tome
0°20′ N 6°44′ E
Mji mkubwa nchini Sao Tome
Lugha rasmi Kireno
Serikali Jamhuri
Carlos Vila Nova
Jorge Bom Jesus
Uhuru
 - Date
Kutoka Ureno
12 Julai 1975

currency = Dobra

Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,001 km² (ya 171)
0% (visiwa)
Idadi ya watu
 - 2021 kadirio
 - 2012 sensa
 - Msongamano wa watu
 
223,107 (ya 186)
178,739
199.7/km² (ya 69)
Fedha {{{currency}}} (STD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
UTC (UTC+0)
(UTC)
Intaneti TLD .st
Kodi ya simu +239

-



Jamhuri ya Kidemokrasia ya São Tomé na Príncipe (kifupi: Sao Tome na Principe) ni nchi ndogo inayoundwa na visiwa vichache vilivyoko katika Bahari ya Atlantiki mbele ya pwani ya Afrika ya Magharibi katika Ghuba ya Guinea. Ilikuwa koloni la Ureno hadi mwaka 1975.

Eneo lake ni hasa visiwa viwili vikubwa vya São Tomé na Príncipe pamoja na visiwa vidogo kadhaa.

Sao Tome na Principe vina umbali wa km 140 kati yake, vikiwa takriban km 250 na 225 kutoka pwani ya Gabon.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]
Ramani ya São Tomé and Príncipe

Visiwa vyote ni vilele vya milima ambayo ni sehemu ya safu za volkeno zilizokua kuanzia sakafu ya bahari hadi kufikia usoni pake. Volkeno hizi ni zimwe, si hai tena.

São Tomé ndicho kisiwa kikubwa, chenye takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi. Kisiwa hicho kina urefu wa km 48 na upana wa km 32. Kimo cha milima yake hufikia mita 2,024 juu ya UB. Sao Tome iko kaskazini kidogo kwa mstari wa ikweta.

Jina la Sao Tome linamaanisha "Mtakatifu Thomas" kwa sababu Wareno walifika huko mara ya kwanza siku ya Mt. Thomas katika kalenda ya Kanisa Katoliki.

Kisiwa cha pili, jina lake ni Príncipe, yaani "Mfalme mdogo" au "Mwana wa mfalme"; kina urefu wa km 16 na upana wa km 6. Milima yake hufikia mita 927 juu ya UB.

Rolas ni kisiwa kidogo kusini kwa Sao Tome chenye wakazi 200 na mstari wa ikweta unapitia humo.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Visiwa hivyo havikuwa na wakazi hadi vilipogunduliwa na Wareno katika karne ya 15.

Baadaye vilikuwa koloni la Ureno kuanzia karne ya 16 hadi 12 Julai 1975, vilipopata uhuru.

Nchi ilifuata siasa ya chama kimoja tangu uhuru hadi mwaka 1990. Katiba ya 1990 imeruhusu vyama vingi.

Rais huchaguliwa na wananchi wote kwa muda wa miaka mitano.

Nchi ina mikoa miwili (inayolingana na visiwa viwili) na wilaya saba. Wilaya sita ziko kwenye kisiwa kikubwa cha Sao Tome na ya saba iko Principe.

Miji mikubwa zaidi ni (takwimu za 2005):

  • São Tomé: wakazi 56.1670
  • Santo Antonio: wakazi 8.239
  • Neves: wakazi 7.392
  • Santa Cruz: wakazi 6.969
  • Trindade: wakazi 6.636

Wananchi wana asili mbalimbali, wakiwemo Waafrika, Wazungu, Machotara na Waasia.

Pamoja na lugha rasmi ya Kireno, inayojulikana na 98.4% ya wakazi wote, wengi hutumika lugha za Krioli zinazochanganya Kireno na lugha za Kibantu kama vile Saotomense (wasemaji 70.000), Principense (wasemaji 1.500) na Angolar (wasemaji 5.000).

71.9 % za wakazi ni Wakatoliki, takriban 10.2 % ni Waprotestanti.

Uchumi wa visiwa ulikuwa hasa mashamba makubwa ya kakao pamoja na kahawa na mazao ya minazi.

Katika miaka ya nyuma akiba za mafuta ziligunduliwa baharini katika maeneo kati ya Sao Tome na Nigeria.

Mwaka 2001 nchi hizo mbili zilipatana kuendelea pamoja na utafiti wa akiba hizo. Kutokana na kazi hizi kuna matumaini ya mapato makubwa wakati ujao.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons

Serikali

[hariri | hariri chanzo]

Uchambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Mazingira

[hariri | hariri chanzo]

Mambo mengine

[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sao Tome na Principe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.