Tamaduni ya Kiafrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Utamaduni wa Afrika inajumuisha tamaduni zote ambazo ziliwahi kuwa katika bara la Afrika.

Mpasuko mkuu ni kati ya Afrika ya Kaskazini (pamoja na Pembe ya Afrika),] ambayo ni sehemu ya Kiislamu , na Afrika ya Sub-Sahara, ambayo imegawanywa katika idadi kubwa ya tamaduni za kikabila. Mikasama kuu ya kikabila ni Afro-Asiatic (Afrika ya kaskazini, Chad, Pembe ya Afrika), Niger-Congo (sanasana Kibantu) katika sehemu kubwa ya Sub-Sahara ya Afrika , Nilo-Saharan katika maeneo ya Sahara na Sahel na sehemu za Afrika ya Mashariki na Khoisan (wazawa wachache wa Afrika Kusini.

Dhana ya utamaduni wa Pan-African ulijadiliwa kwa makini katika miaka ya 1960 na 1970 katika muktadha wa harakati ya Négritude , lakini dhana hii imepoteza mtindo katika masomo ya Afrika. Usambazaji pana wa Kibantu katika Afrika ya Sub-Sahara, unaojumuisha maeneo ya Afrika ya Magharibi, Afrika ya Mashariki, Afrika ya Kati na vilevile Afrika ya Kusini ni matokeo ya upanuzi wa Kibantu wa milenia ya 1 BK. Utumizi pana wa Kiswahili kama lingua franca yaonyesha kwa uzaidi Kibantu kama athari ya tamaduni ya "Pan-African".


Watu[hariri | hariri chanzo]

Asili ya wakazi wengi wa Afrika ni ya wazawa.


Afrika ina makabila mengi ambayo hayawezi kuhesabika na vikundi vya kikabila na vya kijamii. Baadhi ya vikundi hivi vinaashiria wakazi wengi ambao ni mamilioni ya watu. Vikundi vingine ni vikundi vidogo vya watu elfu kadhaa. Baadhi ya nchi zaidi ya makabila 20 tofauti, na pia ni tofauti sana katika imani.


Sanaa na Afrika[hariri | hariri chanzo]

Afrika ina mila tajiri ya sanaa. Sanaa za Africa hujieleza katika aina mbalimbali ya mchongo wa mbao, shaba na matendo ya sanaa ya ngozi. Sanaa ya Afrika pia inajumuisha uchongaji, uchoraji, ufinyanga, mavazi ya mwili na ya kichwa katika sherehe, na mikutano ya kidini.

Utamaduni wa Afrika daima umetilia mkazo vile mtu anavyojitokeza na majohari yamebaki vidude muhimu ya kibinafsi. Vipande vingi vya majohari vimetengenezwa na simbi vifaa kama vya simbi. Vilevile, miundo ya maskhara zinatengenezwa na umakini na ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Afrika. Maskhara hutumika katika sherehe mbalimbali kuashiria mizimu na vizuka, wahusika katika hadithi na miungu.


Katika mila nyingi ya sanaa ya Afrika, baadhi ya mandhari adhimu kwa utamaduni wa Afrika hujirudia kama vile wapenzi wawili, mwanamke na mtoto, mume na silaha au mnyama, na mtu kutika nje au mgeni. Wapenzi wawili wanaweza kuwakilisha mizimu, mwanzilishi wa jamii, wapenzi wawili waliooana au mapacha. Mandhari ya wapenzi wawili adimu huonyesha undani wa wanaume na wanawake. Yule mama na watoto au watoto hufumbua hamu kubwa ya wanawake wa Afrika kupata watoto. Mandhari pia inaashiria mama mirihi na watu kama watoto wake. Mandhari ya mtu na silaha au mnyama mandhari inaashiria fahari na nguvu. Mgeni anaweza kuwa ametokea kutoka baadhi ya makabila au awe mtu kutoka nchi nyingine, na zaidi upotovu wa mgeni huonyesha pengo kubwa kutoka kwa mgeni.


Folklore na dini ya kimila[hariri | hariri chanzo]

Kama tamaduni zote za kibinadamu, "Folklore" ya kiafrika na masimulizi huashiria pande mbalimbali za utamaduni wa Afrika [1] Kama karibu staarabu na tamaduni zote, hadithi za mafuriko zimekuwa zikienea katika maeneo mbalimbali ya Afrika. Kwa mfano, kulingana na hadithi ya chuchu au mtwa (pygmy kwa lugha ya kimombo), kinyonga aliposkia kelele ya ajabu akiwa mtini, shina ya mti huo ulifunguka na maji ilimwagika kama gharika kuu iliyoenea kote ardhini. Wapenzi wa kwanza wa binadamu waliibuka kutoka majini. Vilevile, hadithi moja kutoka Cote d'Ivoire inasema kwamba mhisani mmoja alipatiana kila kitu alichokuwa nacho. Mungu wake, Ouende , alimtuza kwa kumpa utajiri, alimshauri aondoke kutoka eneo hilo, na alituma miezi sita ya mvua kuharibu jirani wake wachoyo.


Lugha[hariri | hariri chanzo]

Bara la Afrika lazungumza mamia ya lugha na kama lahaja zinazozungumza na makabila tofauti zinajumuishwa, idadi ni kubwa zaidi. Lugha na lahaja hizi zote hazina umuhimu sawa: baadhi yao huzungumzwa na watu mia chache tu, zingine huzungumzwa na mamilioni. Kati ya lugha maarufu zaidi zinzozungumzwa ni Kiarabu, Kiswahili na Kihausa. Nchi chache za Afrika hutumia lugha moja na kwa sababu hii, lugha rasmi kadhaa zinatumika, Kiafrika na kiulaya. Baadhi ya Waafrika pia wanaweza kuzungumza lugha mbalimbali kama vile kimalagasi, Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kibambara, Kisotho na mengineo.

Lugha ya Afrika huonyesha umoja wa tabia na vilevile utofauti (diversity), kwani ni wazi katika vipimo vyote vya Afrika. Familia nne maarufu za lugha ni:

  • Afro-Asiatic
  • Nilo-Saharan
  • Niger-Kordofanian
  • Khoisan

Senta ya mapema ya maandiko ilikuwa African Ink Road.

Ramani zinazoonyesha mgawanyo wa familia ya lugha za Afrika na baadhi kubwa lugha za Afrika. Afro kutoka-Kiasia linahusu Afrika Kaskazini kupitia Pembe ya Afrika na Asia ya Magharibi. Niger-Congo ni kugawanywa ili kuonyesha ukubwa wa familia ndogo ya Kibantu.

Kupitia makadirio mengi, Afrika ina ziadi ya lugha elfu. Kuna familia nne kuu za kienyeji za lugha kutokea Afrika.

  • Lugha ya Afro-Asiatic ni familia ya lugha zaidi ya 240 na watu milioni 285 wameenea katika Pembe ya Afrika, Afrika ya Kaskazini, Asia ya Magharibi na maeneo ya Sahel.
  • Familia ya lugha ya Nilo-Saharan inajumuisha lugha zaidi ya mia moja zinazozungumzwa na watu milioni 30. Lugha za Nilo-Saharan hasa huzungumzwa nchini Chad, Ethiopia, Kenya, Sudan, Uganda na kaskazini mwa Tanzania.
  • Familia ya lugha ya Niger-Congo inahusisha sehemu kubwa ya Afrika ya Sub-Saharan na pengine ndiyo familia kubwa ya lugha duniani miongoni mwa lugha nyingine. Idadi yao kubwa ni lugha ya Kibantu inayozungumzwa sana katika Afrika ya sub-Saharan.
  • Lugha za Khoisan zina idadi ya lugha hamsini na zinazungumzwa kusini mwa Afrika na takriban watu 120,000. Baadhi ya lugha nyingi za Khoisan ziko katika hatua ya kutokomea. Jamii za Khoi na San ndizo zinazochukuliwa kama wenyeji asili wa sehemu hii ya Afrika.


Pamoja na nchi chache mashuhuri katika Afrika ya Mashariki karibu nchi zote za Afrika zilisiliki lugha rasmi zilizoasilika kutoka nje ya bara na kuenea kupitia ukoloni au uhamiaji wa binadamu. Kwa mfano, katika nchi mbalimbali, Kiingereza na Kifaransa (angalia Kifaransa cha Kiafrika) hutumiwa kwa mawasiliano katika nyanja za umma kama vile serikali, biashara, elimu na vyombo vya habari. Kiarabu, Kireno, Kiafrikaan na Kimalagasi ni mifano la lugha zisizo za kiasili ya kiafrika ambazo hutumika na mamilioni ya Waafrika leo, katika nyanja za umma na za kibinafsi.


Upishi[hariri | hariri chanzo]

Afrika ni bara kubwa na vyakula na vinywaji vyake hudhania mivuto ya kienyeji, na utumizi wa vyakula vya kikoloni vya kimila, vikijumuisha pilipili , njugu na mahindi, vilivyoanzishwa na wakoloni. Upishi wa Afrika ni mchanganyiko wa matunda na mboga ya kimila, maziwa na bidhaa za nyama. Mlo wa kijiji cha Afrika mara nyingi huwa ni maziwa na bidhaa za maziwa. Wanyama na samaki hukusanywa kutoka eneo kubwa la Afrika.


Upishi wa kimila ya kiafrika inatabia ya utumizi wa Wanga kama umakini, ikifuatwa na kitoweo yenye nyama au mboga, au yote mawili. Mihogo na viazi vikuu ndizo mboga kuu. Waafrika pia hutumia mboga zilizopashwa moto na ambazo zina pilipili. Vyakula vya mboga vilivyopashwa moto au kuchemshwa, mbaazi, maharagwe na nafaka, mihogo, viazi vikuu na viazi vitamu huliwa kwa wingi. Katika kila eneo la Afrika, kuna aina mbalimbali ya matunda ya pori na mboga ambazo hutumika kama chakula. Mtengomaji, ndizi na migomba ni baadhi ya matunda yanayojulikana.


Tofauti hujulikana katika tabia za kula na kunywa barani Afrika. Hivyo, Afrika Kaskazini, pamoja Mediterania kutoka Moroko hadi Misri zina tabia tofauti za chakula kuliko Waafrika wa Sahara ambao hula mlo wa kujikimu. Nigeria na sehemu za pwani za Afrika Magharibi hupenda vyakula vya pilipili. Idadi ya Waafrika ambao si waislamu pia hutumia vileo, ambayo huenda vyema na vyakula vingi vya kiafrika. Pombe inyojulikana sana ndani ya Afrika ni mvinyo kutoka Ethiopia inayoitwa Tej iliyotengenezwa kutumia asali.


Mbinu za kupika za Afrika Magharibi mara nyingi kuchanganya samaki na nyama, pamoja na samaki iliyokaushwa. Upishi wa Afrika Kusini na nchi jirani kwa kiasi kikubwa zinapika vyakula vya machanganyiko, kwa kupata mvuto kutoka wahamiaji kadhaa ambao ni pamoja na Wahindi ambao walileta supu ya adesi,(dals) na muchuzi, Malays waliokuja na michuzi yao ya viungo, na Wazungu na "mixed grills" ambao sasa injumuisha nyama ya wanyama wa Afrika. Kimila, vyakula vya Afrika Mashariki ni tofauti kwa maana kwamba bidhaa za nyama haviko kwa ujumla. Ng'ombe, kondoo na mbuzi walichukuliwa kama aina ya sarafu, na kwa ujumla wanyama hawa hawatumiwi kama vyakula. Mivuto ya Kiarabu yanajitokeza katika upishi wa vyakula vya Afrika Mashariki - mchele uliopikwa kwa viungo katika mtindo fulani, matumizi ya karafuu, mdalasini na viungo vingine vingi, na juisi.


Waethiopia wanadai kuwa wa kwanza kulima kahawa, na wana sherehe za aina nyingi za kahawa , kama sherehe ya chai ya kijapani. Kutoka Ethiopia, kahawa ilienea Yemen, kutoka huko ilienea Arabia, na kutoka huko ikaenea duniani kote.

Marejeleo[hariri | hariri chanzo]