Karanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Njugu)
Jump to navigation Jump to search

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Karanga (Moshi Mjini)

Karanga zilizokauka

Karanga au njugu (kwa Kiingereza: peanut au groundnut) ni mbegu ya mnjugu na moja kati ya mazao muhimu duniani. Jina la Kibiolojia la njugu ni Arachis hypogaea. Vikonyo vya karanga vinaingia katika ardhi na makaka yanaiva hapa chine. Baada ya kukauka makaka haya na matunda ndani yao hufanana na jozi kwa hiyo kuna majina kama "jozi ya ardhini" katika lugha mbalimbali[1] .

Karanga zinaliwa moja kwa moja hasa baada ya kukaangwa, zinasagwa kuwa siyagi ya karanga na hasahasa zinasagwa na kukandamizwa kwa kupata mafuta ya karanga kwa upishi au matumizi viwandani. Mabaki ya karanga baada ya kutolewa kwa mafuta ni lishe bora la nyongeza kwa mifugo kama ng'ombe.

Karanga au mafuta yake zinaweza kusababisha mzio kwa asilimia mdogo wa watu lakini hii ni tatizo katika nchi ambako chakula ni hasa chakula kilichopandaliwa viwandani kutokana na matumizi mapana ya karanga.

Historia ya Njugu[hariri | hariri chanzo]

Kulingana na watafiti wanaoliangazia swala la origin of Groundnuts husemekana kwamba zilitokea nchi ya Argentina, bara la Amerika kusini ambapo njugu ilikuwa ni kama maotea tu.

Sehemu za njugu[hariri | hariri chanzo]

  • Ngozi(shell): hii ni sehemu ngumu ya njugu ambayo huwa inashikana na udongo
  • Kotiledoni: Hii ni sehemu inayolika na huwa mbili unapomega njugu.
  • Ngozi ya mbegu (seed coat): hii ni sehemu nyembamba inayofunika kotiledoni. Huwa na rangi ya kahawia.

Upanzi wa njugu[hariri | hariri chanzo]

Njugu hufanya vizuri katika udongo wa mchanga uliochanganywa na mchanga wa shambani (loamy soil) na wenye PH ya 5.9 hadi 7. Huhitaji hewa yenye joto pamoja na madini ya phosphorus, calcium, magnesium na potassium. Huweza kukua hata kunako mvua kiasi cha 350mm lakini kwa mazao bora huhitaji unyevu wa mvua kiwango 500mm. Njugu huweza kuvunwa baada ya siku tisini baada ya kupanda. Njugu huwa ni moja ya legumes na huweza kuboresha rutuba ya udongo na kwa hiyo huweza kupandwa pamoja na mimea mingine kama vile mahindi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ing. groundnut, jer. Erdnuss, hol. aardnoot, far. بادام زمینی badam zamini, lakini Kiafrikaans grondboontjie "maharagwe ya ardhini"