Nenda kwa yaliyomo

Ufalme wa Muungano

Majiranukta: 55°N 3°W / 55°N 3°W / 55; -3
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ufalme wa Muungano wa Britania
na Eire ya Kaskazini

United Kingdom of Great Britain
and Northern Ireland
Bendera ya Ufalme wa Muungano Nembo ya Ufalme wa Muungano
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: "Dieu et mon droit" (Kifaransa)
"Mungu na haki yangu"
Wimbo wa taifa:

"God Save the Queen"
Lokeshen ya Ufalme wa Muungano
Mji mkuu London
51°30′ N 0°7′ W
Mji mkubwa nchini London
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali
1: Mfalme Ufalme wa Muungano
2: Waziri Mkuu wa Ufalme wa Muungano
bunge la ufalme wa kikatiba wa muungano
1: Charles III wa Uingereza
2: Keir Starmer
'
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
243,610 km² (80th)
1.34%
Idadi ya watu
 - 2019 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
67,545,757 (22nd)
63,181,775
270.7/km² (50th)
Fedha Pound Sterling (£) (GDP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
Greenwich Mean Time (GMT) (UTC+0)
British Summer Time (BST) (UTC+1)
Intaneti TLD .uk
Kodi ya simu +44

-



Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini (kwa Kiingereza: United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland); kifupi: "Ufalme wa Muungano" (Kiing.: United Kingdom) ni nchi ya visiwani ya Ulaya ya kaskazini-magharibi. Mara nyingi huitwa kwa Kiswahili "Uingereza" tu ingawa nchi ya Uingereza ni moja tu kati ya sehemu za ufalme huo pamoja na Uskoti, Welisi na Eire ya Kaskazini.

Katika karne zilizopita nchi iliongoza mapinduzi ya viwanda duniani, ilienea katika mabara yote kwa makoloni yake mengi ikabaki hadi leo kati ya nchi muhimu zaidi ulimwenguni.

Ni mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Mataifa, ambapo ana kiti cha kudumu na kura ya turufu katika Halmashauri ya Usalama.

Miaka 1974-2020 ilikuwa pia ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya; ilijiondoa baada ya kura ya wananchi.

Historia

Eneo hilo lilikaliwa na watu tangu miaka 30,000 iliyopita.

Miaka 2000 iliyopita kisiwa cha Britania kilikaliwa na makabila ya Wakelti kikavamiwa na Dola la Roma kuanzia mwaka 43 BK. Waroma wakatawala sehemu zote za kisiwa kikubwa isipokuwa Uskoti kwa miaka 400.

Walipoondoka wanajeshi wao, walowezi wapya Wagermanik kutoka Ujerumani wa Kaskazini na Denmark walihamia kisiwani, wanaojulikana kama Wasaksoni na Waangli. Utamaduni wa Wakelti uliendelea katika Welisi na Uskoti.

Ndicho chanzo cha Ufalme wa Uingereza uliounganisha sehemu zilizokaliwa na walowezi Wagermanik.

Mwaka 1066 Wanormani kutoka Ufaransa walivamia Uingereza wakafaulu kuchukua utawala wa kusini mwa Uingereza. Uvamizi wao ulibadilisha utamaduni na pia lugha ya nchi. Walifaulu kuvamia Welisi na Uingereza lakini walishindwa kuteka Uskoti. Katika karne za utawala wao lugha ya Kiingereza ilizaliwa ambayo kimsingi bado ni lugha ya Kigermanik ya Wasaksoni pamoja na athira kubwa ya msamiati wa Kilatini-Kifaransa uliotokana na mabwana Wanormani walioshika utawala.

Tangu mwaka 1284 Welisi ilitawaliwa na Uingereza na katika Hati ya Muungano (Act of Union) ya mwaka 1536 ilikuwa rasmi sehemu ya Milki ya Uingereza.

Kutokana na asili yao katika Ufaransa ya kaskazini wafalme wa Uingereza walijaribu pia kutetea madai yao ya utawala juu ya sehemu za Ufaransa. Baada ya Vita ya Miaka 100 walipaswa kuachana na madai haya.

Katika karne ya 16 mfalme Henry VIII aliamua kutanganisha Kanisa Katoliki la nchi yake kutoka mamlaka ya Papa hivyo akweka misingi kwa kutokea kwa Kanisa Anglikana.

Wakati huohuo mfalme wa Uingereza alipanusha utawala wake juu ya kisiwa cha Eire.

Tangu 1603 mfalme wa Uingereza alikuwa pia mfalme wa Uskoti na hati ya Muungano ya mwaka 1707 iliunganisha milki mbili za Uingereza na Uskoti kuwa Milki ya Britania Kuu. Tangu wakati uleule Ufalme wa Eire (Ireland) ilitawaliwa na Uingereza pia.

Katikati ya karne ya 17 kulikuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe ya 1642 hadi 1648. 1649 mfalme Charles I alihukumiwa na kukatwa kichwa na kwenye Mei wa mwaka uleule Uingereza ulitangaziwa kuwa "Commonwealth" yaani jamhuri chini ya Oliver Cromwell. Baada ya kifo chake ufalme ulirudishwa lakini wafalme hawakupata tena utawala kamili walipaswa kukubali kipaumbile wa bunge la raia wa ufalme. Hivyo Uingereza ilikuwa mfano wa mfumo wa utawala wa sheria inayoundwa na wawakilishi wa wanachi wenyewe.

Tangu karne ya 18 Uingereza ilikuwa nchi ya kwanza iliyoona maendeleo ya teknolojia iliyoleta mapinduzi ya viwandani. Utajiri wa uwezo wake ulipanuka na kuweka msingi wake wa kutawala nchi nyingi nje yake kwa mfumo wa ukoloni.

Sheria ya mwaka 1800 iliunganisha Ufalme wa Britania Kuu na Ufalme wa Eire na hivyo kuunda Ufalme wa Muungano (United Kingdom of Great Britan and Ireland).

Baada ya Vita vya uhuru vya Eire bunge la London kwa sheria ya mwaka 1920 (Government of Ireland Act 1920) liligawa Ireland katika sehemu mbili za Northern Ireland na Southern Ireland.

Wabunge waliochaguliwa katika Ireland ya Kusini walijitangaza kuwa bunge la Eire na kwa mapatano ya mwaka 1922 uhuru wa Eire ulitambuliwa. Nchi mpya ilijiita tangu 1937 "Jamhuri ya Eire" na kuendelea kama nchi ya pekee. Mikoa ya Northern Ireland iliendelea kuwa sehemu za Ufalme wa Muungano.

Mwaka 1999 Uskoti, Welisi na Ireland ya Kaskazini zilirudishiwa mabunge yao ya pekee.

Uskoti ulikuwa na harakati pana ya kuondoka katika Ufalme wa Muungano lakini katika kura ya watu wa Uskoti ya mwaka 2014 asilimia 55 waliamua kubaki.

Kumbe kura ya wananchi wa Ufalme mzima ya mwaka 2016 iliamua kuondoka katika Umoja wa Ulaya kwa asilimia 51.9. Utekelezaji ulihitaji muda mrefu na kutimizwa tarehe 31 Januari 2020.

Wakazi

Wenyeji wengi wana asili ya Kigermanik na ya Kiselti, lakini uhamiaji mkubwa umeleta Wazungu wengine wengi na kufanya sasa 7% wawe na asili ya Asia, 3% wana asili ya Afrika, 2% ni machotara, n.k.

Upande wa lugha, Kiingereza ndiyo lugha mama ya 94.5% za wakazi na kinatumika kama lugha rasmi hata bila kutangazwa.

Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2011, 59.5% za wakazi ni Wakristo (hasa wa Anglikana, halafu Wakatoliki, Wamethodisti, Wakalvini na wengineo), 4.4% ni Waislamu, 1.3% ni Mabanyani, 0.7% ni Singasinga, 0.4% Wayahudi, 0.4% Wabuddha n.k. 25.7% hawana dini yoyote.

Muungano na utawala

Bendera Nchi Hali Wakazi Vitengo Mji mkuu
Uingereza Ufalme 50,431,700

Mikoa
Wilaya

London
Uskoti Ufalme 5,094,800

Wilaya

Edinburgh
Welisi Utemi 2,958,600

Wilaya

Cardiff
Hapana Eire Kaskazini Jimbo 1,903,100

Wilaya

Belfast

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Serikali
Taarifa za jumla
Utalii


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ufalme wa Muungano kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

55°N 3°W / 55°N 3°W / 55; -3