Uhispania : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 180: Mstari 180:
[[Jamii:Nchi za Umoja wa Ulaya]]
[[Jamii:Nchi za Umoja wa Ulaya]]
[[Jamii:Mkataba wa Schengen]]
[[Jamii:Mkataba wa Schengen]]
[[Jamii:Umoja wa Forodha wa Ulaya inaanzishwa]]
[[Jamii:Umoja wa Forodha wa Ulaya]]
[[Jamii:Nchi za Ulaya]]
[[Jamii:Nchi za Ulaya]]
[[Jamii:Nchi zinazotumia Kihispania]]
[[Jamii:Nchi zinazotumia Kihispania]]

Pitio la 22:42, 13 Desemba 2020

Uhispania


Hispania (kwa lugha ya wenyewe: España, kwa Kiingereza Spain) ni nchi ya Ulaya ya kusini-magharibi. Imepakana na Ufaransa, Andorra, Ureno na eneo la Kiingereza la Gibraltar.

Kuna pwani ndefu ya Bahari ya Mediteranea na pia ya Atlantiki.

Hispania bara ni sehemu kubwa ya rasi ya Iberia. Visiwa vya Baleari kwenye Mediteranea na Visiwa vya Kanari katika Atlantiki pamoja na miji ya Afrika ya Kaskazini Ceuta na Melilla ni sehemu za Hispania.

Mji mkuu ni Madrid ambayo ni pia mji mkubwa wa nchi.

Eneo la nchi ni km² 500,000 nalo lina wakazi 46.733.038 (2018).

Mfalme Felipe VI amevaa taji mwaka 2014, akishika nafasi ya baba yake Juan Carlos I, anayeheshimiwa sana kwa sababu aliongoza taifa katika mabadiliko ya kutoka udikteta wa jenerali Francisco Franco kuelekea demokrasia. Hasa tendo la mfalme la kuzuia mapinduzi wa kijeshi linakumbukwa sana.

Muundo wa serikali ni Ufalme wa Kikatiba, hivyo kisheria madaraka ya mfalme ni madogo.

Utawala umo mikononi mwa serikali inayochaguliwa na bunge linaloitwa "Las Cortes likichaguliwa kwa kura za kidemokrasia.

Historia

Historia ya awali

Wakazi wa kwanza waliojulikana kwa jina kuwa waliishi Hispania walikuwa Wakelti.

Wafoinike

Katika karne za KK Wafoinike walianzisha miji kwenye pwani na kuchimba madini hasa shaba na fedha.

Waroma

Waroma wa Kale walivamia na kutawala Hispania kwa karne kadhaa wakileta lugha yao ya Kilatini kilichopata kuwa msingi wa lugha za kisasa za Hispania. Kibaski pekee si lugha ya Kirumi.

Katika karne ya 5 makabila ya Kigermanik walivamia Dola la Roma pamoja na Hispania. Kati yao Wavandali na Wavisigothi walitawala sehemu kubwa ya Hispania.

Waarabu

Tangu mwaka 711 jeshi la Waarabu Waislamu liliingia kutoka Afrika ya Kaskazini na kutwaa sehemu kubwa ya Hispania hadi karibu milima ya Pirenei, lakini watawala wa maeneo kadhaa katika kaskazini walijihami na kufaulu kudumisha uhuru wao.

Waarabu walileta fani nyingi za maendeleo nchini.

Katika kipindi cha vita cha karne nyingi Wakristo wa Kaskazini walifaulu polepole kuwarudisha nyuma Waarabu hadi kusini kwa nchi.

Hatimaye mwaka 1492 mfalme Boabdil wa Granada, mji wa mwisho wa Waarabu, alishindwa na mfalme Ferdinand II wa Aragon na malkia Isabella wa Kastilia.

Makoloni ya Amerika

Wiki chache kabla ya kushinda huko Granada wafalme wa Hispania walimkubalia nahodha Kristoforo Kolumbus kutafuta njia ya kufika Bara Hindi kupitia magharibi. Badala ya kufika India Kolumbus alifika kwenye visiwa vya Amerika ya Kati.

Huo ulikuwa mwanzo wa upanuzi wa Hispania katika "Dunia Mpya" ya Amerika. Wahispania walijenga dola kubwa la kikoloni na kutwaa karibu Amerika ya Kusini yote pamoja na Amerika ya Kati na Mexiko hadi sehemu za kusini za Marekani ya leo.

Katika miaka mia tatu iliyofuata Hispania ilitajirika sana kutokana na maliasili ya Amerika.

Vita vya Marekani dhidi ya Hispania

Vita hivyo vilitokea mwaka 1898. Vilianza kwa shambulizi la Marekani tarehe 25 Aprili dhidi ya Puerto Rico vilivyokuwa koloni la Hispania na kuishia tarehe 12 Agosti 1898, jeshi la Hispania huko Manila (Ufilipino) liliposalimu amri.

Vita hivyo vilikuwa mwanzo wa Marekani kufuata siasa ya nje ya upanuzi hata katika maeneo ya mbali. Kabla ya vita hivyo Marekani ilishughulika kupanua eneo lake kwenye bara la Amerika ya Kaskazini dhidi ya wakazi asilia na dhidi ya Mexiko.

Marekani ilitumia nafasi ya ghasia ya wenyeji wa Kuba dhidi ya utawala wa kikoloni wa Hispania.

Baada ya mlipuko kwenye manowari ya Marekani USS Maine katika bandari ya Havana, Marekani ilitangaza vita dhidi ya Hispania ingawa sababu ya mlipuko haijajulikana hadi leo ilikuwa nini.

Hispania haikuweza kushindana na manowari na silaha za Marekani zilizokuwa zimeendelea kiteknolojia.

Pia Marekani ilikuwa karibu na mahali pa vita na Hispania ilishindwa kuongeza wanajeshi na silaha.

Hivyo Marekani ilitwaa makoloni ya Hispania ya Puerto Rico, Kuba na Ufilipino.

Jiografia

Ramani ya Hispania

Miji mikubwa

Watu

Wakazi walio wengi (89.67%) ni Wahispania asili, lakini uhamiaji mkubwa wa miaka ya mwisho umeleta watu wengi hasa kutoka Amerika ya Kilatini, Afrika Kaskazini, Ulaya Mashariki n.k.

Lugha rasmi ni Kihispania inayozungumzwa nyumbanin na 74% za watu lakini majimbo 17 yamepewa mamlaka ya kujitawala katika mambo mbalimbali pamoja na sera za kiutamaduni hivyo lugha za Kikatalunya (17%), Kigalicia (7%), Kibaski (2%) na Kioccitan zimekuwa lugha rasmi za kijimbo pamoja na Kihispania.

Wahispania walio wengi (67%) ni waamini wa Kanisa Katoliki. 25% hawana dini yoyote.

Picha

Tazama pia

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Ramani
Utalii


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uhispania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.