Jumuiya ya Afrika ya Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
EAC Flag
Nchi tano za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki

Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (East African Community - EAC) ni ushirikiano kati ya nchi tano za Afrika ya Mashariki, hususan Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi na Rwanda.

Jumuiya hii imepatikana mara mbili katika historia:

Jumuiya ya kwanza[hariri | hariri chanzo]

Nchi tano za Afrika ya Mashariki zilizokuwa chini ya utawala wa Uingereza na Ubelgiji zilianza uhuru wao kwa ushirikiano wa karibu uliorithiwa kutokana na utawala wa pamoja wa kikoloni. Baada ya kupata uhuru mwaka 1961 nchi tatu ziliunda Mamlaka ya Huduma za Pamoja za Afrika ya Mashariki (East African Common Services Organisation – EACSO).

Ushirikiano ulihusu fedha (East African Shilling), forodha (Customs Union), huduma za reli (East African Railway), ndege (East African Airways), mabandari, posta na simu na elimu ya juu (Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki chenye kampasi Makerere, Daressalaam na Nairobi). Mkataba ulilenga pia kwa mahakama kuu ya pamoja na siasa ya kiuchumi ya soko la pamoja. Haya yote yalitakiwa kuwa chini ya Bunge la Afrika ya Mashariki.

Tangu 1965 umoja huu ulianza kurudi nyuma kila nchi ilipoanzisha pesa yake. Mwaka 1967 nchi tatu zilijaribu upya kuimarisha umoja wao kwa Mkataba wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki wakiita umoja wao "Jumuiya ya Afrika ya Mashariki“ ikiwa makao makuu ndipo Arusha.

Lakini mielekeo ya nchi zote tatu zilitofautiana mno, Kenya ikiendelea kwa njia ya upebari lakini Tanzania ilijaribu kujenga Ujamaa (usoshalisti) kuanzia mwaka 1967. Uganda uliingia katika kipindi cha udikteta kali ya Idi Amini aliyeharibu uhusiano na majirani alipoanza kudai sehemu za maeneo yao.

Hivyo mwaka 1977 Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ilikoma kufanya kazi yoyote na 1983 ilifutwa rasmi. Mali iliyobaki iligawanywa kati ya nchi zote tatu.

Kufufuka kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki tangu 1993[hariri | hariri chanzo]

Tangu miaka ya 1990 majaribio ya kunjenga umoja mpya yalionekana tena. Marais Moi wa Kenya, Mwinyi wa Tanzania, na Museveni wa Uganda walipatana Mkataba wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki huko Arusha, Tanzania, tarehe 30-11-1993.

Jumuiya mpya ya Afrika ya Mashariki ilianzishwa Januari 2001 huko Arusha – Tanzania penye makao makuu ya jumuiya hii. Mkataba wa 2004 uliweka msingi wa Umoja wa Forodha ulioanzishwa 2005.

Kuna tena Bunge la Afrika ya Mashariki linalojumuisha wabunge waliochaguliwa na mabunge ya nchi wanachama.

Pia Mahakama Kuu ya Afrika ya Mashariki imeundwa upya.

Kuna mipango kuwa tena na pesa ya pamoja.

Nchi wanachama[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]