Shilingi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shilingi ni pesa inayotumika kwa malipo halali katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, na maeneo ya mipaka ya nchi za Maziwa Makuu, Zambia, Malawi, na Msumbiji.

[hariri] Historia ya Shilingi

Asili yake ni kitengo cha kihistoria cha pesa ya Uingereza iliyoitwa "Shilling". Hadi 1971 Pauni 1 ya Kiingereza ilikuwa na shilling 12 na kila shilling ilikuwa na penny 20.

[hariri] Shilingi ya Afrika ya Mashariki

Uingereza ilitoa "East African Shilling" kuanzia 1921 kama pesa ya pamoja kwa ajili ya koloni zake za Kenya, Uganda na Tanganyika. Zanzibar ilijiunga na shilingi hii mwaka 1935 ilipoacha rupia zake. Baada ya uhuru nchi hizi zilivunja umoja huu zikaanzisha pesa zao za pekee. Zote zinaitwa shilingi lakini thamani ilianza kuwa tofauti haraka.

Kuna majadiliano ya kurudisha shilingi ya pamoja kwa nchi za Afrika ya Mashariki.

WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Shilingi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Shilingi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.