Idi Amin
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Idi Amin Dada alikuwa rais wa Uganda kati ya 1971 hadi 1979 aliyetawala kama dikteta.
Alikuwa mwanajeshi akapanda ngazi kuwa jenerali na mkuu wa jeshi la Uganda. 1971 alimpindua rais Milton Obote akajitangaza kuwa rais mpya.
Mara moja alianza kuwatesa wafuasi wa Obote na watu wote waliompinga. Kuna makadirio ya kwamba jumla ya watu 100,000 hadi 500,000 waliuawa katika miaka nane ya utawala wake.
Aliharibu uchumi wa Uganda kwa ufisadi na majaribio ya kuongoza biashara. Hatua kubwa ya uharibifu ilikuwa kufukuzwa kwa watu wote wenye asili ya Kihindi na kugawa kwa maduka na biashara yao kwa ndugu au wafuasi wa rais. Takriban watu 80,000 walipaswa kuondoka kwao wakihamia Uingereza, Marekani au Kanada hasa.
Oktoba 1978 Amin alianzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuvamia sehemu za mkoa wa Kagera. Rais Julius Nyerere wa Tanzania aliamua kumwondoa Amin kabisa na jeshi la Tanzania likatwaa Kampala tar. 11 Aprili 1979.
Amin alitoroka Libya, halafu Irak na mwishowe Saudia alikopewa kimbilio kwa masharti ya kutoshughulika siasa tena.
Alikufa mjini Jeddah tar. 16 Agosti 2003.
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Idi Amin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |