Nenda kwa yaliyomo

Makanisa Katoliki ya Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wakatoliki wa mashariki)
Askofu Mkatoliki wa Mashariki akiadhimisha Liturujia ya Kimungu huko Prešov (Slovakia).

Makanisa Katoliki ya Mashariki ni madhehebu 23 ya Ukristo ambayo yanafuata mapokeo mbalimbali ya Mashariki katika ushirika kamili na Askofu wa Roma (Papa), hivyo pia na Kanisa Katoliki lote duniani.

Mapokeo hayo ni hasa yale ya Aleksandria (Misri), Antiokia (kihistoria jiji la Siria, leo nchini Uturuki), Konstantinopoli (kihistoria jiji la Ugiriki, leo nchini Uturuki), Armenia na Wakaldayo (kihistoria Mesopotamia, leo Iraq).

Baadhi ya mapokeo hayo yamezaa matawi, kama ya Misri yale ya Ethiopia na Eritrea.

Pamoja na hayo, kama Makanisa ya Waorthodoksi, hayo pia yanaambatana na utamaduni wa taifa, na kuyafanya yagawanyike kiutawala hata kama teolojia, liturujia n.k. zinaendelea kuwa zilezile kadiri ya mapokeo.

Kwa jumla yanakubali kuwa mapadre watu waliooa lakini hawana maaskofu waliooa.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Shamba la Mungu la Wakatoliki wa Mashariki huko Pennsylvania (Marekani).
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Chanzo cha Wakatoliki wa Mashariki ni tofauti: baadhi (hasa wale wa Kanisa la Wamaroni) wanadai kuwa wamedumu tangu mwanzo katika ushirika kamili na Papa, au walijikuta hawana tena mawasiliano na Patriarki wao kutokana na hali ya siasa, hivyo wakaanza kushirikiana na Kanisa la Kilatini (hasa Kanisa la Waalbania wa Italia). Wengine wametokana na makubaliano kati ya Papa na baadhi ya Waorthodoksi walioona umuhimu wa kuwa na umoja naye, hata wakakubali kutengana na Makanisa yao ya asili (kwa mfano Kanisa Katoliki la Kisiria la Malankara).

Kwa mengine mengi ni kwamba siku za nyuma kulikuwa na majaribio mbalimbali ya Mapapa ya kuunganisha Makanisa ya Kiorthodoksi na Kanisa la Roma baada ya mafarakano yaliyotokea hasa katika karne ya 5. Majaribio hayo kwa jumla yalishindikana, lakini pengine yalisababisha mafarakano mapya katika makanisa ya Kiorthodoksi ambamo askofu fulani alikubali mamlaka ya Papa na kuungana na Kanisa la Roma pamoja na wafuasi wake. Mara kadhaa hao walikuwa wanagombea vyeo vikuu katika Makanisa ya Kiorthodoksi, halafu wakaamua kuungana na Papa baada ya kutochaguliwa katika makanisa yao ya asili. Kwa sababu hiyo, wanatazamwa vibaya na Waorthodoksi.

Siku hizi Kanisa Katoliki limetamka wazi kwamba halina tenga mipango kama hiyo katika kulenga umoja na madhehebu mengine, bali linafuata njia za ekumeni.

Mtaguso wa pili wa Vatikano uliyazungumzia Makanisa Katoliki ya Mashariki na kuyatolea hati "Orientalium Ecclesiarum" ili yastawi upya na kuwa daraja kati ya Wakatoliki na Waothodoksi.

Kuna Makanisa 23 yaliyounganika hivyo na Roma. Kati ya hayo makubwa zaidi ni:

Katika Afrika yako hasa Makanisa ya:

Leo Wakatoliki wa Mashariki ni asilimia 1.5 ya Wakatoliki wote, yaani kwa jumla kuna walau Wakristo milioni 18 katika makanisa hayo.

Kati yao wengi wanafuata mapokeo ya Kigiriki, Kimesopotamia na ya Kisiria.

Kwa kawaida Makanisa hayo yangetakiwa kuongozwa na Patriarki, lakini upinzani wa Waorthodoksi umefanya Papa asiyapatie cheo hicho yale yasiyokuwa nacho tayari. Badala yake kilibuniwa kile cha Askofu mkuu kabisa, ambacho kina mamlaka karibu sawa katika madhehebu makubwa 4: Waukraina, Wasiro-Malabari, Wasiro-Malankara na Waromania.

Mengi ya makanisa haya yanakubali kuwapa upadri waamini waliooa, lakini maaskofu na sehemu ya mapadri hawaoi. Kwa kawaida wanachagua maaskofu wao wenyewe watakaothibitishwa na Papa, tofauti na Wakatoliki wengi katika Kanisa la Kilatini ambako ni Papa anayemteua askofu mpya moja kwa moja.

Katika nchi kadhaa Makanisa mbalimbali ya Kikatoliki yanaishi kandokando, kwa mfano Misri kuna Kanisa la Kikopti-Katoliki, la Kigiriki-Katoliki, la Kiarmenia-Katoliki, la Kikaldayo-Katoliki na la Kilatini.

Mapadri (lakini si maaskofu) Wakatoliki wa mapokeo ya Kikopti, ya Kigiriki, ya Kiarmenia na ya Kikaldayo wanaweza kuwa na ndoa na huendesha Misa katika taratibu zao za kale; kumbe mapadri Walatini hawawezi kuwa na ndoa na hufuata liturujia ya Roma.

Wote hao hukubali uongozi wa Papa bila kushindana, yaani wengine wanahudumia Wakatoliki wa mapokeo ya Kikopti, wengine wale wa mapokeo ya Kigiriki, wengine wale wa mapokeo ya Kiarmenia, wengine wale wa mapokeo ya Kikaldayo na wengine wale wa mapokeo ya Kiroma, hasa wahamiaji kutoka nchi nyingine.

Nchi ambazo zina makao makuu ya Kanisa fulani la Kikatoliki ya Mashariki (nyekundu: mapokeo ya Kigiriki; kijani kibichi: mapokeo ya Aleksandria; manjano: mapokeo mengine).

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

Kwa jumla

[hariri | hariri chanzo]

Moja moja

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Makanisa Katoliki ya Mashariki kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.