Kanisa Katoliki la Kigiriki la Romania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanisa kuu la Utatu Mtakatifu la jimbo la Blaj.
Kanisa la Mediaş.
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Waamini huko Transilvania (1850)
Waamini huko Romania (1930)
Waamini huko Romania (2002)
Uwepo wa waamini nchini kadiri ya sensa ya mwaka 2002[1]
Majimbo nchini

Kanisa Katoliki la Kigiriki la Romania (kwa Kiromania Biserica Română Unită cu Roma, Greco-Catolică) ni mojawapo kati ya madhehebu ya Ukristo wa mashariki yenye ushirika kamili na Papa na Kanisa Katoliki lote.

Linafuata mapokeo ya Ukristo wa Ugiriki na kutumia liturujia ya Ugiriki likiongozwa na Askofu mkuu kabisa, kwa sasa kardinali Lucian Mureşan.

Mbali ya jimbo kuu la Fǎgǎraş na Alba Iulia, nchini Romania kuna majimbo manne: Oradea Mare, Cluj-Gherla, Lugoj na Maramureş.[2]

Kanisa hilo lina pia jimbo la Mt. George huko Canton, Marekani linalowashughulikia waamini walioko Amerika Kaskazini, ikiwa ni pamoja na Canada.[3]

Kadiri ya Annuario Pontificio ya mwaka 2016, mwishoni mwa mwaka 2012 Kanisa hilo lilikuwa na waamini 504,280 katika parokia 1225, wakiongozwa na maaskofu 8 na mapadri wanajimbo 882 hivi, ingawa sensa iliyoendeshwa na serikali ya Romania mwaka 2011 ilidai waamini waliokuweko nchini walikuwa 150,593 tu.[4][5]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Baada ya Austria kuteka Transilvania mwaka 1687, askofu mkuu Atanasie Anghel alikubali kuungana na Kanisa la Roma mwaka 1698, na uamuzi huo ulipitishwa na sinodi ya maaskofu tarehe 4 Septemba 1700.[6]

Baada ya Ukomunisti kuteka Romania, ulilazimisha waamini wote wa Kanisa hilo kujiunga tena na Waorthodoksi, lakini wengine walikataa na kuendelea kufuata imani yao kwa chinichini, bila ya kujali dhuluma iliyoendelea hadi tarehe 31 Desemba 1989.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Source: http://recensamant.referinte.transindex.ro/ Archived 20 Machi 2012 at the Wayback Machine.
  2. "Romanian Catholic site". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-07-23. Iliwekwa mnamo 2013-07-07. 
  3. Romanian Catholic Eparchy of St George's in Canton
  4. 2002 Romanian census official data.
  5. International Religious Freedom Report 2005 United States Department of State
  6. The Harper Collins Encyclopedia of Catholicism (New York: Harper Collins, 1995) 1132.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanisa Katoliki la Kigiriki la Romania kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.