Nenda kwa yaliyomo

Kanisa la Wamaroni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Kirusi ya Mt. Maroni.
Peshitta ni toleo sanifu la Biblia ya Kiaramu. Picha inahusu Kut 13:14-16 ilivyoandikwa huko Amida mwaka 464.
Mmonaki wa Kimaroni na waamini waliofika kwa hija kwenye Mlima Lebanoni.
Mmonaki wa kike wa Kimaroni kutoka Mlima Lebanoni, alivyochorwa mwaka 1779.
Wanakijiji Wamaroni wakijenga kanisa kwenye Mlima Lebanoni, miaka ya 1920.
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Kanisa la Wamaroni (kwa Kilatini Ecclesia Maronitarum; jina rasmi: Kanisa la Kisirya la Kimaroni la Antakya; kwa Kiaramu ܥܕܬܐ ܣܘܪܝܝܬܐ ܡܪܘܢܝܬܐ ܕܐܢܛܝܘܟܝܐ ʿīṯo suryaiṯo māronaiṯo d'anṭiokia; kwa Kiarabu الكنيسة الأنطاكية السريانية المارونية al-kanīsa al-antākīyya al-seryānīyya al-mārwnīyya) ni moja ya Makanisa Katoliki ya Mashariki, yaani ni Kanisa linalojitegemea kisheria ndani ya umoja wa Kanisa Katoliki.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mzizi wake ni katika Kanisa la Kisirya la Kiorthodoksi kwenye nchi za Syria na Lebanoni za leo, kwa hiyo katika utamaduni wa Wakristo waliotumia lugha ya Kiaramu cha magharibi.

Kanisa hilo lilianza katika mvutano juu ya maamuzi ya Mtaguso wa Kalsedonia wa mwaka 451 yaliyokataliwa na Wasirya wengi. Wafuasi wa mmonaki Maroni, mwanzilishi wa monasteri maarufu katika karne ya 4, walisimama upande wa maazimio ya huo mtaguso mkuu ingawa walikuwa Wasirya. Kwa hiyo Wamaroni waliteswa na wenzao wakawa kundi la Wasirya waliosimama upande wa Kanisa la Kigiriki la Kiorthodoksi.

Katika mabishano yaliyofuata ndani ya Kanisa la Kigiriki Wamaroni waliamua kukaa kando, wakawa jumuiya ya pekee na kutafuta hifadhi yao kwenye milima ya Lebanoni.

Wakati wa vita vya msalaba Wamaroni walielewana vizuri na Wakatoliki kutoka Ulaya wakatafuta ushirikiano nao. Hapo walikubali uongozi wa Papa wa Roma na kuwa hadi leo Kanisa pekee la Ukristo wa Mashariki lililopo lote chini ya Papa.

Hali ya leo[hariri | hariri chanzo]

Wamaroni wanatunza liturujia, teolojia na maisha ya kiroho ya mazingira hayo kulingana na tapo lililoanzishwa na Maroni. Hadi leo sehemu za liturujia ziko kwenye lugha ya Kisirya au Kiaramu cha magharibi lakini kwa jumla Kanisa na pia jumuiya ya Wakristo wake hutumia Kiarabu.

Patriarki wake anachaguliwa na Sinodi ya maaskofu wa Kanisa hilo, halafu anamuomba Papa wa Roma ushirika kamili. Anaishi Bkerke (Lebanoni), ambapo ana jimbo lake, ingawa anatumia bado jina rasmi la Patriarki wa Antiokia.

Kanisa hilo linakubali kuwapa upadri waamini waliokwishaoa.

Uenezi[hariri | hariri chanzo]

Huko Lebanoni, ni kundi kubwa, ingawa wanazidi kupungua kwa sababu ya matatizo yanayowafanya wengi kuhamia nchi nyingine.

Wanakaribia kuwa 3,500,000 duniani kote [1], wakiishi katika majimbo 28 kama yafuatavyo.

Huko Lebanoni: Zahleh, Tiro, Tripoli, Sidoni, Joubbeh - Sarba - Jounieh (jimbo la Patriarki), Jbeil - Byblos, Beirut, Batrun, Baalbeck - Deir el Ahmar na Antelias

Huko Syria: Latakia, Damascus na Aleppo.

Huko Israel: Haifa - Nchi Takatifu.

Katika nchi nyingine: Afrika Magharibi na ya Kati (Ibadan, Nigeria), Brooklyn (Marekani), Buenos Aires (Argentina), Cairo (Misri), Cyprus, Kolombia, Los Angeles (Marekani), Mexico, Montreal (Canada), Paris (Ufaransa), Sao Paulo (Brazil), Sudan na Sydney (Australia).

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Moosa, Matti, The Maronites in History, Gorgias Press, Piscataway, NJ, 2005, ISBN 978-1-59333-182-5
  • R. J. Mouawad, Les Maronites. Chrétiens du Liban, Brepols Publishers, Turnhout, 2009, ISBN 978-2-503-53041-3
  • Kamal Salibi - A House of Many Mansions - The History of Lebanon Reconsidered (University of California Press, 1990).
  • Maronite Church. New Catholic Encyclopedia, Second Edition, 2003.
  • Riley-Smith, Johnathan - The Oxford Illustrated History of the Crusades (Oxford University Press, Oxford, 1995)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Wamaroni kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.